Home Kitaifa BILIONI 25.4 KUTUMIKA KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 374 JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

BILIONI 25.4 KUTUMIKA KUSAMBAZA UMEME VITONGOJI 374 JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Bunda-Musoma

KIASI cha shilingi bilioni 25.4 kimetengwa kwa shughuli ya usambazaji umeme.kwenye vitongoji 374 vilivyopo kwenye vijiji 68 vya jimbo la Musoma vijijini.

Kauli hiyo imetolewa jana agosti 8 na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sosperer Muhongo wakati akielezea shughuli ya usambazaji wa umeme itakayoanza jumatatu ya agosti 12.

Amesema REA na TANESCO wanayo maombi ya kusambaziwa umeme kwenye vitongoji hivyo na mipango inayoendelea na utasambazwa kwa awamu endelevu.

Muhongo amesema upo mradi wa vitongoji 68 kila Kata ambapo mradi huo unatekelezwa sasa kwenye (Lot V)

Mbunge huyo amesema viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji wanapaswa kuwa na orodha ya maeneo yao
kuanza kusambaza nguzo kupitia mkandarasi Alpha TND Ltd

Amesema upo mradi wa Vitongoji 15 ambapo
mradi huu ni utekelezaji wa ahadi ya Wizara ya Nishati kwa wabunge wote kila jimbo litasambaziwa umeme kwenye Vitongoji 15 mkandarasi ikiwa kampuni ya
Dieynem Co Ltd

“Mkandarasi anaendelea kufanya tathmini ya Vitongoji 30 na kati ya hivyo 15 vitachaguliwa kusambaziwa umeme kutumia fedha zitakazotolewa.

“Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji vyetu waendelee kushirikiana na Afisa wa REA (W) na wakandarasi wote wawili kwenye utekelezaji wa miradi hii miwili ya usambazaji wa umeme kwenye vitongoji vyetu.

“Kwa sasa jumla ya Vitongoji 83 (68+15) vitasambaziwa umeme na tunaendelea kufuatilia maombi yetu hadi vitongoji vyote 374 viunganishiwe umeme”, amesema

Kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini na Viongozi wao mbalimbali Muhongo ameishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendele kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ya usambazaji umeme wa bei nafuu kwenye vitongoji vyao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!