Home Kitaifa BIBI MLEZI WA WATOTO YATIMA BUKOBA AILILIA SERIKALI, WADAU KUMSAIDIA VIFAA VYA...

BIBI MLEZI WA WATOTO YATIMA BUKOBA AILILIA SERIKALI, WADAU KUMSAIDIA VIFAA VYA KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA 2 ZA KUISHI WATOTO ANAOWALEA

Theophilida Felician, Kagera

Bibi Saada Seleman mkazi wa kata ya Hamgembe Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera mlezi watoto yatima katika kituo cha UYACHO kilichopo kata ya Hamgembe Manispaa ya Bukoba ameiomba Serikali na wadau wengine kumshika mkono na kumsaidia vifaa vya kukamilisha nyumba mbili anazozijenga ili kuishi watoto yatima anaowalea kituoni kwake UYACHO.

Akizungumza na Blog hii ya Mzawa bibi Saada anakojenga nyumba hizo kitongoji cha Katongo Kijiji cha Mbale Kata Kitobo Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera amesema kuwa amefikia hatua ya kuanzisha ujenzi wa nyumba hizo baada ya kituo cha awali UYACHO kulemewa na idadi kubwa ya watoto ambapo kwa sasa anao watoto 290.

“Baada yakuona idadi ya watoto inaongezeka kituo kile nikaona bora nianzishe ujenzi wa nyumba hizi ili zikikamilika niwapunguze kule baadhi yao niwahamishie hapa ila sasa ndo hivyo nguvu yangu imekwamia hapa nyumba hizi nimeanza ujenzi wake mwaka huu hii moja ya wavulana nimeipandisha nakufikia kiwango cha kuezekwa imekwama mabati, madirisha na milango, nyumba ya wasichana imekwama ikiwa kwenye msingi nasikitisa sana mimi hapa nimezeheka, ni mlemavu wa miguu natambaa nawaza sana naiomba Serikali na wadau, jamii waniunge mkono niweze kukamilisha nyumba hizi nipate pakuwaweka wanangu mfano nikifarika muda huu nawaacha wapi na hali gani?” Ameeleza bibi Saada.

Bibi huyo mwenye umri wa miaka 89 kwa mjibu wa maelezo yake amefafanua kuwa eneo anakojenga nyumba hizo lenye ukubwa wa heka 20 alilikabidhiwa Mnamo mwaka 2010 na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera Kanali Fabian Massawe ambaye alishafariki Dunia.

Amesema kuwa Massawe alimpatia eneo hilo baada ya kufika kituoni kwake UYACHO nakujionea hali halisi ya kitendo cha kiungwana anachokifanya bibi huyo cha kusaidia kuwalea watoto yatima jambo lililompelekea kwenda kumpa eneo hilo ili akafanyie shughuli za kilimo, ufugaji nanyinginezo kwa malengo ya kuwasaidia chakula watoto wale.

Hata hivyo maelezo yake zaidi yamejikita kuwaomba viongozi wa Serikali ngazi mbalimbali kuwiwa nakulifikia eneo hilo ili kuijonea hali ilivyo.

“Mkuu wetu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya Misenyi na Mkuu wa wilaya ya Bukoba niwaombe mnifike hapa mnione mnipambanie nipate vifaa hivyo tuwasaidie watoto hawa nimeishahangaika nimeishaomba huku nakule lakini bado nimekwama mno” ameendelea kubainisha kwa msisitizo bibi huyo.

Hata hivyo ameongeza kuwa watoto anaowalea wengine huwapokea kutoka ustawi wajamii huku wengi wao wakiwa hatika hali ngumu kiafya kutokana na mazingira wanayokutwa nayo.

Amehitimisha akimuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelea kumpumzisha kwa amani Kanali Fabian Massawe kwani bado anaishi na kumbukumbu yake kutokana na mchango wakumpatia eneo hilo ambalo linaendelea kuwa msaada kwa katika mambo mbalimbali ya mahitaji ya watoto.

Baadhi ya wananchi wa kitongoji hicho liliko eneo la bibi saada akiwemo Emenueli Richard, Dominick Mchunguzi, na Samweli Mulio awali ameshukuru nakupongeza jitihada za bibi huyo kwakujitolea kuwalea watoto yatima licha ya changamoto zake za ulemavu na uzee lakini bado anapambana kuhakikisha watoto wanaotaabika maeneo tofauti tofauti anawalea kwa namna yoyote ile.

Pia nao wameiomba Serikali, wadau na jamii kwa ujumla kumsadia kwa namna mbalimbali mlezi huyo aweze kujenga nyumba hizo ambazo zimekwama ujenzi wake mpaka sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!