Home Kitaifa BI. LILIAN MTALI ATUA TANZANIA COMMERCIAL BANK ( TCB ) KWA...

BI. LILIAN MTALI ATUA TANZANIA COMMERCIAL BANK ( TCB ) KWA KISHINDO

 Na Mwandishi Wetu.

Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) inayo furaha kumkaribisha Bi Lilian Mtali kuwa Mkurugenzi wa Biashara kwa wateja Wadogo na wa Kati,  Bi. Mtali ana uzoefu wa miaka 26 katika sekta ya huduma ya kifedha akibobea katika usimamizi na uongozi wa huduma za biashara za wateja wateja wadogo, wa kati na wakubwa.

Bi. Mtali amefanya kazi na kupata uzoefu wa uongozi kutoka benki mbalimbali za hapa nchini na za kimataifa, amefanya kazi katika benki za I&M Bank Tanzania Limited,  Standard Chartered, Stanbic na DCB akishika nyadhifa mbalimbali za uongozi kama Meneja wa tawi, Mshauri wa Masuala ya Fedha (Personal Financial Consultant, Meneja Uhusiano wa Wateja (Priority banking) , Meneja wa Huduma kwa Wateja na Ubora wa Huduma na Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa Wateja Wadogo na Wakubwa.

Katika utendaji wake, Bi. Mtali amefanya mabadiliko makubwa katika ukuaji na maendeleo ya taasisi zote alizofanya kazi amesimamia miradi mbalimbali ya kibenki kwa ujumla ikiwemo kuongeza wigo wa mikopo ya biashara kwa wateja wadogo, kusimamia ukuaji wa wateja binafsi (High Valued Customers), kusimamia ukuaji wa huduma za uwakala usimamizi, na mikopo ya kidigitali.

Bi.  Mtali amekuwa nguzo ya uongozi katika kuleta mabadiliko chanya ya taasisi na kuchochea mabadiliko ya uendeshaji biashara na utendaji wa taasisi.

Bi. Mtali ana Shahada ya Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo cha Kimataifa cha Amerika (IUA), London Campus, United Kingdom na Cheti kutoka Modern Tutorial College London, United Kingdom. Aidha, amesoma kozi na semina mbalimbali za uongozi wa kimataifa kutoka United Kingdom, Afrika Kusini, Kenya, Zimbabwe, Angola na Singapore. 

Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Bwana Adam Mihayo akiongea kuhusu ujio wa Bi. Lilian Mtali katika Benki ya TCB alisema ana imani na uzoefu mkubwa wa Bi. Mtali pamoja na uwezo wake wa uongozi hivyo ni matumaini yao kwamba atakuwa msaada mkubwa wakati huu ambao benki iyo  inalenga kuboresha huduma za wateja wa rejareja, wadogo na wa kati.

Taarifa hii imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Tanzania Commercial Bank (TCB).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!