Mhe.Cleopa Msuya (Waziri mkuu mstaafu, mshauri na mwanahisa wa benki ya Mwanga Hakika) akizungumza na wanahisa kwenye mkutano mkuu wa pili uliofanyika 27-08-2022 Wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Mwanga Hakika,Eng.Ridhiwani Mringo akizungumza na wanahisa wa benki ya Mwanga Hakika,wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
……………………………………………………..************************************………………………………………………….Na Mwandishi Wetu.Kilimanjaro, Mwanga. Benki ya Mwanga Hakika yafanya mkutano mkuu wa pili na wanahisa wa benki
hiyo yaani AGM (Annual General Meeting) wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro, kwenye ukumbi wa
Baobab Retreat Hall, siku ya Jumamosi 27 Agosti 2022.
Mkutano huu una lengo la kutimiza sharia ya nchi, itakayo kila kampuni kufanya mkutano mkuu na
wanahisa wao kila mwaka. Mbali na hayo,mkutano huo ulikuwa na lengo la kuimarisha uhusiano uliopo
baina ya wanahisa hao na benki hiyo, ili kuwataarifu wanahisa hao kuhusu benki hiyo ilipotoka, ilipo na
pia inapokwenda ili kuweza kupata taarifa kamili na Ili wanahisa hao waweze kutathmini maendeleo ya
benki hiyo na kubaini changamoto ili ziweze kutatuliwa. Na waweze kutoa ushauri juu ya maswala ya
kimaendeleo yatakayo ikuza benki hiyo na kuwa imara zaidi.
Mkutano huu ni mkutano wa pili na wanahisa wa benki ya Mwanga Hakika, ambapo mkutano wa
kwanza ulifanyika mwaka jana (2021) na kuhudhuriwa na wanahisa mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha
uhusiano wao na wanahisa wa benki hiyo. Pia mikutano hii ina chachu ya kukutanisha wanahisa kwa
pamoja na kudumisha umoja na mshikamano wao.
Mbali na hayo, benki ya Mwanga Hakika imefanya mkutano huo wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro
kwasababu benki hiyo chimbuko lake ni Mwanga ambapo ilianzishwa mnamo mwaka 2000, ikiwa
inaitwa Mwanga Community Bank (Benki ya Wananchi Mwanga) na baadhi ya wanahisa waliohudhuria
mkutano huo ni waasisi, kwani walikuwepo tangia benki hiyo ilipokuwa change. Na kama wasemavyo
Waswahili “Mcheza Kwao Hutuzwa”. Benki ya Mwanga Hakika inatambua hilo na kuenzi msemo huo.
Mkutano huo uliohudhuriwa na Wanahisa zaidi ya 300, wakiwemo waasisi na viongozi mbalimbali wa
benki hiyo nao ni, Eng.Ridhiwani Mringo ambaye ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa benki ya
Mwanga Hakika, pia Mhe.Cleopa Msuya(Aliyekuwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu Mstaafu, Mwanahisa
wa benki ya Mwanga Hakika, na mshauri wa benki hiyo), Eng. John K Msemo (Mkurugenzi) CPA (T) Zukra
Ally (Mjumbe wa bodi) Bw. Christopher Mageka (Mkaguzi wan je wa mahesabu), Mwakilishi kutoka
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Leodgara A. Haule na wengine wengi.
Kabla ya mkutano huo kulikuwa na semina na wanahisa, ambapo waliweza kutoa maoni, pongezi na
kutaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya benki hiyo miaka ijayo. Pia Mjumbe wa bodi CPA (T) Zukra Ally,
alitoa elimu ya uwekezaji kwa njia ya hisa, na alieleza kuhusu gawio la wanahisa, ununuaji na uuzaji wa
hisa, na kueleza baadhi ya sheria zinazoongoza benki hiyo. Na kusema kuwa “Sheria ya mapato (2004)
inayodhibiti masuala ya teknolojia na tehama sababu mabenki yanakuwa na mtandao mkubwa ila
kupitia sharia hizi kunakuwa na siri baina ya mabenki na watu wao”.
Na aliongeza kuwa, “Katika ulimwengu wa leo, kampuni zenye hisa ndio chombo madhubuti ya
kuwekeza biashara,mradi tu kuwepo na uimara wa bodi,menejiment ya wwenye taaluma ya biashara
husika kama ifanyavyo benki ya Mwanga Hakika, hivyo msisite kuweka hisa zenu’’.
Ambapo mmoja kati ya wanahisa hao, Bwana. Josephat Shirima alisema kuwa “Nipende kupongeza
uongozi wote wa benki ya Mwanga Hakika kwa tukio hili linaonyesha kuwa mnatambua mchango wetu,
ningeomba pia kama kuna uwezekano tawi mojawapo liwe ni kwa jina la Mhe. Cleopa Msuya, ili
kuonyesha kwamba tunatambua mchango wake kwenye benki hii,kwani amepigana vema tangu benki
hii ilipokuwa benki ya Wananchi hadi hivi leo”.
Kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa benki ya Mwanga Hakika, Eng. Ridhiwani
Mringo, alieleza mapato na matumizi kwa mwaka ulioishia 31 Disemba 2021, utekelezaji wa mpango wa
biashara kwa mwaka mmoja uliopita, na kuteua wajumbe wa bodi kwa mwaka 2021/2022.
Mbali na hayo,kwenye mkutano huo yalijadiliwa mapendekezo kutoka kwa wanahisa, na mwanahisa
mmoja aliipongeza benki na alipendekeza benki kuongeza mawakala wa kutosha, pia kuongeza
matangazo, ili benki ijulikane vizuri.
Pia, Mhe.Cleopa Msuya, Waziri Mkuu mstaafu, alitoa historia fupi ya jinsi walivyoanzisha Mwanga
Community Bank (Benki ya Wananchi Mwanga) na kusema kuwa “Tulipoanzisha benki hii tulikuwa na
lengo la kuwa benki ya jamii, na nipende kumpongeza Mwenyekiti wa Bodi pamoja na bodi yake kwa
kazi kubwa walioifanya na naomba muendelee na kazi nzuri ambayo mmeianzisha, vilevile nipende
kuwaomba wanahisa wote kutafakari jinsi benki hii inavyowasaidia kimaendeleo”.
Aliongeza kuwa “Nipende kuomba benki hii iendelee na mchakato wa kuwa benki kubwa ya biashara, na
isisahau kuhudumia wateja wadogo wadogo ambao ndio walikuwa lengo kuu la kuanzishwa wka benki
hizi za kijamii”.
Na Mwakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Leodgar A. Haule, aliipongeza benki kwa kufanya
vizuri kwa kipindi cha muda mfupi na aliipongeza kwa mtaji ambao umepata hadi kufikia hatua ya kuwa
benki ya biashara. Na kusema kuwa “Nipende kuwapongeza wote,hasa uongozi wa benki ya Mwanga
Hakika pamoja na wanahisa wote kwa juhudi mzifanyazo kuhakikisha benki hiyo inapata maendeleo
zaidi, pia niiombe benki hii iendelee kufanya kazi kwa bidi na kufuata sheria mbalimbali zilizopo.
Aidha, alisema kuwa, Benki Kuu, itaendelea kusimamia na kutoa ushauri kwa benki kama msimamizi
mkuu wa Mabenki nchini.