Home Kitaifa BEI YA NISHATI SAFI YA GASI IPUNGUE ILI HATA FAMILIA DUNI ZIWEZE...

BEI YA NISHATI SAFI YA GASI IPUNGUE ILI HATA FAMILIA DUNI ZIWEZE KUACHANA NA MATUMIZI YA NISHATI YA KUNI NA MKAA TUTUNZE MAZINGIRA – DR. MWAMPOGWA

Na Scolastica Msewa, Kibaha.
Mkurugenzi Mtendaji Jukwaa la Wazalendo huru Dk. Mohamed Mwampogwa ameomba serikali kuendelea kupigania kupungua kwa bei ya gasi ili hata zile familia duni ziweze kushiriki kampeni hizi za kutunza mazingira kwa kutumia gasi badala ya kuni na mkaa.

Amesema hayo katika zoezi la upandaji miti katika viwanja vya shule ya msingi Mwakamo na Sekondari ya Samia Mtongani katika Kijiji cha Kisabi Mlandizi kibaha mkoani Pwani.

Amesema matumizi ya nishati ya kuni na mkaa ni makubwa nchini hivyo ilikunusulu mazingira yetu kwa kubadilika na kutumia nishati safi ya gasi.

Dr. Mwampogwa amesema ni bora watanzania kupika kwa kutumia nishati safi ya gasi badala ya kuendelea kutumia kuni na mkaa ambayo inaendelea kuharibu mazingira na inatishia Hali ya nchi yetu.

“Matumizi ya kuni na mkaa nchini ni makubwa sana na kupelekea kuendelea kuharibu mazingira yetu kwani kuni na mkaa hutokana na miti ya misitu yetu hivyo tutaokoa mazingira yetu “ alisema Mwampogwa.

Amepongeza Mheshimiwa Rais Samia kwa jitihada zake kubwa anazoendelea kuzifanya katika kutunza mazingira na kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa salama muda wote.

Akizungumzia Jukwaa hilo la Wazalendo huru kuhusu upandaji miti amesema wamepanda Miche ya miti 300 katika shule mpya ya msingi Mwakamo na Sekondari ya Samia Mtongani huko Mlandizi kibaha mkoani Pwani ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kutunza mazingira.

Mwampogwa amesema miti iliyopandwa ni miti ya matunda, miti ya vivuli na miti ya mbao zoezi ambalo ni endelevu kwani tayari wamependa miti hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

“Jukwaa limeamua kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM taifa lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi”

“Sisi Wazalendo huru tunaelekea pia kuhamasisha jamii ya watanzania kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa wingi katika maeneo yao yanayowazunguka ili kwa pamoja tutunze mazingira” alisema.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Jukwaa la Wazalendo huru amewataka Viongozi na wanachama wa Jukwaa hilo kuendelea kupanda miti kwa wingi katika maeneo mikoa, wilaya zao ili kuendelea kutunza mazingira katika taifa letu.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania Yahya Calamba amesema jukwaa hilo limepanda miti 300 katika eneo la shule hizo ili kulinda eneo hilo na uaribifu wa mazingira.

Ameagiza miti hiyo itunzwe na kulindwa ili kurudisha uoto wa asili katika eneo hilo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wazalendo huru taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo mkoa wa Pwani Hadija Juma amesema wiki hii taifa lipo katika wiki ya mazingira wakachagua shule hizo mbili.

Amesema jukwaa hilo limechagua kujikita katika upandaji miti ilikuhakikisha taifa linapandwa miti ilikutunza mazingira.

Hadija amesema upandaji miti huo pia ni sehemu ya sherehe za Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa hilo la Wazalendo huru tarehe 23 mwezi huu anatarajia kutunukiwa nishani ya udaktari wa heshima kwa kazi nzuri anazoendelea kuzifanya nchini.

Amesema wanachama na Viongozi wa jukwaa hilo wanaendelea kumuombea kwa Mungu ili aendelee kuifanyia kazi tuzo hiyo kuhudumia wananchi hadi maendeleo yapatikane katika jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!