OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa Kituo kipya cha Mabasi Katesh katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Akizungumza wakati wa ziara yake akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Hanqng leo 26, Septemba 2022. Bashungwa amesema kasi ya Mkandarasi Erelai Construction Company Limited wa Arusha ni ndogo na itasababisha mradi huo kutokukamilika kwa wakati uliopangwa.
Waziri Bashungwa amesema kuwa Serikali tayari imetoa kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kuanza ujenzi tangu mwezi Feburuari, mwaka huu lakini mpaka sasa ujenzi huo una sua sua na kulingana na Makubaliano ya Mkataba.
“naagiza ikiwa mkandarasi ameshindwa kufanya kazi atolewe na awekwe mkandarasi mwingine atakayekamilisha kazi kwa wakati ili wananchi kuweza kunufaika na matunda ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan”, ameagiza Mhe. Bashungwa
Vile vile, Bashungwa amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Manyara kuhakikisha anasimamia kitengo cha manunuzi hasa katika suala zima la kuwapata wakandarasi wenye uwezo kwa kuangalia weledi na uzalendo katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Aidha, Ameviagiza vitengo vya manunuzi vihakikishe vinachambua kwa kina wakandarasi wanaoomba kazi za ujenzi ili kuwapata wenye weledi wa kifanyakazi kwa thamani ya fedha inayotolewa iendane na kazi iliyofanyoka.
Mradi umekamilika kwa asilimia 27 ambapo ulianza kutekelezwa 25 Feburuari, mwaka huu na kutakiwa kukamilika mnamo 25 Feburuari, 2023.