Na Mariam Muhando-Dar es salaam.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewataka wadau wa mifumo ya chakula Barani Afrika AGRF kuanza kuainisha maeneo muhimu ya uwekezaji ili kuifanya sekta hiyo kuvutia kwa watu wengi ikiwemo kundi la vijana.
Akizungumza wakati wa kuzindua mpango mkuu wa maendeleo wa mifumo ya chakula 2030 uliofanyika jijini Dar es Salaam, Waziri Bashe amesema
uboreshaji wa mifumo ya chakula 2050 unapaswa kulingana na maono ya maendeleo ya mwaka na dhamira yake utaonekana Agosti mwaka huu.
“Nadhani sasa hadithi na majadiliano ya maendeleo ya kilimo lazima yaingizwe katika mifumo ya chakula lengo ni kutaka kuhamasisha pia kundi la vijana ambalo linahitaji kuwezesha kiteknolojia, fedha na uhakika wa masoko huo ndio mwelekeo wa serikali” alisisitiza Waziri Bashe.
Pia Waziri Bashe amezitaka Nchi za Afrika kuwa na sera nzuri za uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kuharakisha maendeleo ya sekta hiyo na kukuza uchumi wa Afrika.
Katika Uzinduzi huo masuala mbalimbali yamezungumzwa katika mahojiano ya Waandishi wa Habari yalihusisha uzinduzi wa kitabu cha dira ya Ajenda 10/30 chenye lengo la ya uwekezaji kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kukuza kilimo chenye tija nchini Tanzania.
Mkakati wa kitabu hicho pia una shabaha ya kuweka malengo kabambe ya ukuaji wa uchumi kwa muongo ujao ikiwa ni pamoja na kuchochea ukuaji wa kilimo kufikia asimilia 10 ifikapo mwaka 2030.