Home Kitaifa BASHE AMSIMIKA NYIHITA KUWA MLEZI TAASISI YA VIJANA YA KILIMO KWANZA MKOA...

BASHE AMSIMIKA NYIHITA KUWA MLEZI TAASISI YA VIJANA YA KILIMO KWANZA MKOA WA MARA

Na Shomari Binda-Musoma

WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe amemsikika Nyihita Willfred Nyihita kuwa mlezi wa taasisi ya Tanzania Youth Agro Irrigation Development Netwerk Programme kwa mkoa wa Mara.

Licha ya Bashe kumsimika ulezi huo ametoa wito wa kutoachiwa pekee yake shughulu ya uhamasishaji wa vijana kujiunga na kilimo.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Bashe,Afisa Kilimo mkoa wa Mara, Bitrikwa Razalo kabla ya kusimikwa ulezi huo amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameamua kuwashika vijana kupitia kilimo na kuwataka vijana kupokea.

Amesema mkoa wa Mara unao mlango wa kupata masoko ya kilimo ikiwemo migodi,uhifadhi na nje ya nchi ambapo vijana watafanya biashara ya mazao yao.

Bashe amesema ekali 500 ambazo vijana wa mkoa wa Mara wanaweza kuanza nazo na kufanya vizuri wakati wakiendelea kutafuta maeneo mengine.

“Tutaendelea kufanya ufatiliaji wa karibu na wa kutosha kupitia maagis kilimo ili kuhakikisha malengo yaliuokusudiwa yanafanikiwa”

“Kuhusu upungufu wa maeneo niwaombe viongozi wa serikali kwenye wilaya za mkoa wa Mara kutoa maeneo yaliyo wazi bila vikwazo ili mambo yaende” amesema.

Akizungumza mara baada ya kusimikwa nafasi ya ulezi wa taasisi hiyo anakwenda kufanya kilimo kuwa ajira kwa vijana wa mkoa wa Mara.

Amesema anashukuru kwa nafasi hiyo na kuipongeza serikali ya Rais Samia kwa jitihada ambazo zimewekezwa kwenye kilimo na ni muhimu kumuunga mkono.

Nyihita pia amemshukuru Waziri Bashe kwa kusimamia vizuri sekta ya kilimo na kuendelea kupata mafanikio kadri siku zinavyozidi kwenda.

Mlezi huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kiwanda cha Nyihita Sunflower amewataka vijana kuongeza maarifa zaidi ili kuweza kufanikiwa.

“Kama mlezi wa vijana naamini kwa mkoa wa Mara tutafanikiwa kwenye sekta ya kilimo kwa kuwa aliyepewa ulezi ni mtu sahihi”

“Nataka nitembee na vijana wenye uchungu wa kutaka kufanikiwa kwenye sekta ya kilimo na wale wazembe hatuwezi kwenda nao”, amesema Nyihita.

Amesema mkoa wa Mara bado una vijana wavivu na na wanaotaka kufanya siasa wakati wote na kuwataka kubadilika na kuwahakikishia taasisi ya Tanzania Youth na vijana wote wanakwenda kufanya kazi yenye tija.

Awali mratibu wa Taasisi hiyo wilaya ya Musoma Paul Joseph amesema kwa sasa taasisi hiyo ina vijana 300 na wanaendelea kuwahamasisha vijana.zaidi kujiunga na taasisi hiyo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!