Baruti haitakiwi kuhifadhiwa kwenye makazi ya watu kwasababu inaweza kulipuka kwa moto, joto, tayari moto wa gesi au umeme.
Hayo yamesemwa na Mhandisi Mgodi wa Geita Gold Mines GGM Katambala Abeli wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Banda la Chamber of mines huko Dodoma kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Madini mwaka 2024 katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete convention center.
Amesema kwasababu wapo kwenye wiki ya madini ambapo hukutanishwa na Wachimbaji wameona wazungumzie hatari iliyo katika baruti.
“Baruti ni moja ya nyenzo kuu inayotumika kuvunjia miamba migodini, katika Mgodi hauwezi kuvunja miamba mpaka utumie baruti” alisema Katambala.
“Baruti ina madhara makubwa isipohifadhiwa katika mazingira na hali stahiki kama sheria za nchi zinavyoonyesha kwani haitakiwi kuwekwa pamoja na makazi ya watu kwani inaweza kuripuka“