Baraza maalumu la manispaa ya ubungo limemfukuza mtumishi mmoja wa idara ya uhasibu Edga Msuya kwa makosa aliyoyatenda.
Hayo yamesemwa kwenye kikao maalumu kilichofanyika luguruni manispaa ya ubungo ambapo baraza limemridhia mtumishi Mboka Mwelugaja apelekwe kwenye mamlaka yake ya kinidham TSC ili ikashuhulikie tuhuma za ushiriki wa ununuzi wa gari bovu kwa kikundi cha kiuchumi ambacho kilikopeshwa milioni 70
Aidha baraza hilo limewarudisha kazini watumishi wengine ambao wamebainika hawana makosa na kumtaka mkurugenzi wa manispaa hiyo kuandika barua kwa katibu mkuu yakuwaondoa watumishi hao katika manispaa ya ubungo ili kupunguza kasoro mbalimbali kwenye idara ya mikopo ya asilimia kumi
Hata hivyo baraza limewachukulia hatua za kunidhamu watumishi waliobainika na makosa kwenye taarifa ya CAG iliyofanywa kwa miaka 3 ndani ya manispaa.
Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa ya ubungo Beatrice Dominic amesema hatovumilia mtumishi yeyote anayechezea fedha za umma au kushindwa kusimamia miradi.