Na Magreth Mbinga
Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala leo septemba 27 limekaa kwaajili ya kupokea na kupitia taarifa za hesabu za mwisho ambapo sheria inazitaka mamlaka ya Serikali za mitaa kila mwaka wa fedha unapoisha kuandaa taarifa ambayo inahesabu za mwisho za Halmashauri .
Akizungumza kwa niaba ya baraza hilo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Ilala Mhandisi Amani Mafuru amesema takwa la kisheria linataka hesabu za Halmashauri ziwe zinamfikia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali miezi mitatu baada ya mwaka wa fedha kumalizika.
“Sisi Halmashauri vya Jiji la Dar es Salaam tulikamilisha hesabu hizo na zikapitiwa na kamati ya ukaguzi jana tulikuwa na kikao cha kamati ya fedha ,utawala taarifa hizo zikawasilishwa katika kamati ya fedha na utawala ambao inajumuisha baadhi ya Madiwani ambao wanawakilisha wenzao ” amesema Mhandisi Mafuru.
Aidha Mhandisi Mafuru amesema amesema baada ya taarifa hizo kupitiwa Halmashauri imewasilisha taarifa ya hesabu za mwisho katika kikao cha baraza la madiwani.
“Madiwani wameipokea na kupitia kadili walivyoona inafaa wamepitisha ili iweze kuwasilishwa kwa Mshibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa muda uliopangwa kwa maana ya septemba 30 tunashukuru waheshimiwa madiwani wameipokea na wameipitisha na wameiridhia iweze kufikishwa kwa CAG” amesema Mhandisi Mafuru.