Home Kitaifa BARAZA LA MADIWANI, HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME, LIMEAZIMIA KUMUONDOA KAZINI MTUMISHI...

BARAZA LA MADIWANI, HALMASHAURI YA WILAYA YA SAME, LIMEAZIMIA KUMUONDOA KAZINI MTUMISHI MMOJA KWA TUHUMA ZA KUGUSHI VYETI

Na Ashrack Miraji, Mzawa Online

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Same limeazimia kumuondoa kazin Hellen Sige, aliyekuwa Bibi Afya wa Kata ya Hedaru, kwa tuhuma za kugushi vyeti vyake. Uamuzi huo ulifikiwa mwishoni mwa wiki hii wakati wa kikao cha kawaida cha baraza.

Azimio Hilo limewekwa bayana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same,Yusto Mapande ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Msindo, alimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Jimson Mhagama kutekeleza makubaliano yaliyowekwa kuhusu kuondoka kwa mtumishi huyo, pamoja na hatua ya kutoa vishikwambi kwa Madiwani ili waweze kutuma taarifa zao kwa urahisi. Alisisitiza kuwa mipango ya kuifanya baraza kuwa la kielektroniki iendelee kuungwa mkono na watendaji wa Halmashauri

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kaslida Mgeni, alichukua fursa hiyo kuipongeza Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Same, akisisitiza umuhimu wa usimamizi mzuri wa mapato na miradi ya maendeleo. Aliwapongeza Madiwani na watumishi wa umma kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhakikisha kuwa mapato ya Halmashauri yanakusanywa na kutumika ipasavyo.

“Ni furaha yangu kuwaona Madiwani na watumishi wa umma mkiendelea kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa. Hii ni dhihirisho la juhudi zenu katika kusimamia miradi ya maendeleo. Halmashauri yetu inafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato Mkoani Kilimanjaro, na hili linajionyesha wazi,” alisema Mkuu wa Wilaya.

Aidha aliendelea kusema kuwa, kwa msaada wa Rais, Wilaya ya Same imepata fedha zaidi ya bilioni 58 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kwamba ni muhimu Madiwani waendelee kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu miradi inayoendelea katika maeneo hayo

Katika kuzungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mkuu wa Wilaya alitoa wito kwa Madiwani na wananchi wote kushiriki kikamilifu katika uchaguzi unaokuja, akisema kuwa uchaguzi huo ni muhimu kwa maendeleo ya Same na nchi kwa ujumla.

“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni sehemu muhimu katika mchakato wa uchaguzi mkuu mwakani. Hakuna sababu ya kushindwa katika maeneo yetu, kwa sababu Mhe. Rais ameleta mabadiliko makubwa na miradi ya maendeleo. Mnahitaji kufanya kampeni kwa ustaarabu na kwa kuheshimiana, tukizingatia haki za kila mmoja,” alisema.

Mkuu wa Wilaya aliwasisitizia Madiwani kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo katika kata zao, akieleza kuwa katika maeneo ambapo wanakutana na changamoto, wanapaswa kuwasiliana ili kutafuta suluhu za haraka kwa ajili ya ustawi wa wananchi.

“Tutakapokuwa na mshikamano, tutafaulu katika kusimamia miradi ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wetu. Kazi yenu ni kubwa, na tunahitaji kushirikiana ili kufanikisha malengo yetu,” alisema Mkuu wa Wilaya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!