Na Magrethy Katengu
Bandari ya Dar es salaam imepokea Meli kubwa ya Norwegian Line Dawn ya Utalii yenye urefu wa mita 294 aina ya NCL yenye uwezo wa kubeba watu zaidi ya 4700 na imefika Tanzania na Watalii 2210 na wahudumu wa meli 1000 ikitokea bandari ya Mombasa
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es salaaam Mrisho Selemani Mrisho amesema meli hiyo ni kubwa kupokelewa tangu kupata Uhuru kwani hii yote ni kutokana na maboresho makubwa yanayofanywa ikiwemo kuongeza kina cha bahari na magati hivyo kupitia hiyo wanatarajia kupokea Meli nyingine kubwa zaidi kutoka nchi mbalimbali kuleta mizigo abiria.
“Meli hii imeingia asubuhi saa kumi na moja alfajiri Januari 16 2024 sisi tunafurahia sana kwani kampeni ya Royal tour Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imekuja na mafanikio makubwa ya kuleta watalii hawa ambao wengine wanaelekea selou kutalii na vivutio vingine hivyo tumewahudumia vizuri kuanzia walipotoka mpaka walipofika asubuhi wengine wanaendelea kutalii hapa Dar es salaam wakiendelea na safari kwenda Msumbiji” amesema Mriasho
Sisi matarajio yetu ni kuhudumia meli zenye urefu wa mita 305 kwani serikali ya awamu ya sita imeendelea na maboresho makubwa na Bandari ya Dar es salaam ikiwemo kuongeza kina cha bahari na magati yake
Naye wa huduma na Uratibu wa shughuli za Bandari pia ni Nahodha Mkuu wa Meli Abdula Mwingamno amesema bandari hiyo inahudumia meli za abiria mizigo na kontena hivyo wiki tatu zilizopita tumeenda Ujermani kupata mafunzo ya kuingiza meli kubwa ikiwemo eneo hili lililoboreshwa kwani tunataka ushindani wa kibaishara mkubwa
“Hatukupata shida yoyote wakati tunaingiza meli hii kubwa kwa mara ya kwanza yenye urefu ya mita 294 na aliyekuwa anaongoza meli hii aliisifia bandari yetu kuwa defender nzuri ya kuingiza meli hivyo tunathibitisha kuwa serikali inaendea na maboresho yake ikiwemo kuwapeleka wataalamu wengi nje ya nchi ili huduma tuendelee kutoa kwa ufanisi na weledi” amesema Abdula
Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Damasi Mfugale amesema Serikali jitihada zake za kuboresha miundombinu matunda yanaonekana kwani bado kuna meli nyingine ya watalii inatarajiwa kuja hivi karibuni.