Home Kitaifa BANANGA AZITAKA ASASI JIJINI DAR ZIFUNDISHE JAMII KUKATAA RUSHWA

BANANGA AZITAKA ASASI JIJINI DAR ZIFUNDISHE JAMII KUKATAA RUSHWA

Katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es salaam Ally Bananga amezitaka Asasi za Kiraia zilizo katika mkoa huo katika utendaji wa shughuli zao za kila siku katika jamii waongezee jukumu la kutoa elimu ya kupinga vitendo vya rushwa katika jamii inayowazunguka hususani kipindi hiki kuelekea chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

Amesema hayo katika hafla fupi ya sherehe ya maadhimisho ya miaka miwili ya program ya badili tabia sepesha Rushwa iliyoambatana na mahafali ya kwanza ya wanafunzi 150 mabalozi wa Sauti wapinga rushwa Tanzania (ACVF AMBASSADORS) iliyofanyika Ubungo plaza jijini Dar es salaam.

Amesema Asasi hizo ziunge mkono jitihada za serikali katika kupinga vitendo vya rushwa nchini kwa kuongeza hatua nyingine ya utendaji wa shughuli zao ikiwa ni pamoja na shughuli yao ya kujihusisha na kumpamba Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utendaji wake waongezee jukumu la kutoa elimu ya kupinga vitendo vya rushwa katika jamii inayowazunguka.

Bananga amesema taasisi hiyo ya ACVF wao wamejipambanua kivyao kwa kupambana na rushwa na dhuruma wakati taasisi zingine zikifanya machagizo kwa serikali na Rais wetu kumpamba sasa waongeze hatua moja ya kutoa elimu ya kupinga vitendo vya rushwa.

Aliongeza kuwa “Tunapoelekea chaguzi za serikali za mitaa Asasi za CHAMATA, WAMATA, Wazarendo huru na nyinginezo mnapo kwenda kwenye mitaa muende na ujumbe wa wazi kwamba rushwa ni adui wa haki yaani hata wale wanaokwenda kuchaguliwa wajue kwamba rushwa ni adui wa haki tangu wanaingia kuchaguliwa wajue kwamba hata sisi tunaowachagua tunapinga Rushwa”

Hata kwenye nguo mnazovaa pamoja na ujumbe za taasisi zenu lakini pia muweke na ujumbe wa kuonyesha mnapinga vitendo vya rushwa wazi wazi kwasababu najua kila mahali nyinyi mpo hakikisheni mnaisaidia nchi, jamii na mnaunga mkono jitihada za kupinga vitendo vya rushwa nchini”

Amesema malengo ya kuundwa kwa CCM katika katiba yake ibala ya tano msitari wa 16 inasema kuhusu kuona hakuna vitendo vya rushwa, uonevu, au upendeleo ambapo pia katika ahadi za wanachama ahadi namba nne inasema rushwa ni adui wa haki kwamba sitopokea wala kutoa rushwa ambapo pia kaatika kipengele cha uongozi kifungu cha 18 inasema kupokea mapato ya kificho au kupokea / kutoa rushwa hiyo ni miiko ya kiongozi.

Ukimuona kiongozi anafanya hayo hiyo ni tabia yake kwamba CCM kinakataa wazi wazi katika ahadi zake masuala ya rushwa na ndio maana TAKUKURU imeundwa na serikali ya CCM lakini hata mahakama ya mafisadi imeundwa na serikali ya CCM“.

Kaimu RTO Kinondoni ASP Notker Kilewa amekiri kwamba jeshi la polisi limekuwa likilalamikiwa kwa vitendo vya kutoa na kupokea rushwa lakini ameitaka jamii kutokuwa sababiosho la kuchochea vitendo vya kutoa na kupokea rushwa kwa kuzingatia na kutii sheria za nchi.

Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kinondoni Devota Mihayo amesema kipindi cha cha chaguzi sio kipindi cha wagombea na viongozi pekee bali ni kipindi cha wote maana kipindi hicho ndio kinatoa viongozi kwani ndio kipindi ambacho wananchi hujiamulia nani awaongoze katika kipindi cha mika mitano inayokuja.

Niwaombe msikubali kupokea chochote kwa kusema huyu ni mwenyekiti wa mtaa ndiye huwa katika ngazi ya karibu kabisa katika jamii na ndio hutumika kuwezesha kupatikana kwa diwani, mbunge na mstakabali wa maendeleo ya taifa kwa ujumla hivyo ni lazima tuanze kuipinga rushwa hapo na Hii elimu tukaitoe kwenye jamii kwakushirikiana na mabalozi wetu” alisema Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Kinondoni.

Awali Katibu wa taasisi ya Wanafunzi Mabalozi wa Sauti Wapinga Rushwa Tanzania Ezekiel Lesikar amesema taasisi hiyo inampango wa kutoa elimu katika jamii kuhusu kupinga vitendo vya rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!