Na Magrethy Katengu
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Muhammad wa sita ya Maulamaa wa bara la Afrika wametangaza rasmi kuanza mashindano ya kuhifadhi Qurani kwa ngazi ya Afrika yanayotarajiwa kuanza 11 -16 Agosti mwaka huu katika Viwanja vya msikiti Muhammad I VI Dar es salaam nchini Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakari Zuberi ambapo amesema mashindano hayo yatajumuisha hifadhi Qurani na kusoma kwa Tajweed ambapo Washiriki wa mashindano hayo watashindania kupata nafasi tatu Bora kutoka katika vipengele Hifadhi Qurani nzima kwa riwaya Warsh,Qurani nzima kwa Qiraa na riwaya tofauti,kusoma kwa Tajweed lakini kwa uchache mshiriki awe amehifadhi Hizbu tano (Juzuu mbili na nusu)
“Mashindano haya yatafanyika kuanzia siku ya Alhamisi,Ijumaa,Jumamosi,na jumapili tarehe ya 13-14-15-16 Muharram 1444H ambayo ni sawa na tarehe 11,12,13,14 Agosti 2022″ yatahudhuriwa na viongozi na wajumbe wa Taasisi ya Muhammad VI kutoka katika nchi 34 za Afrika pamoja na washiriki 88 ambao ni Wanachama” amesema Sheikh
Hata hivyo amesema Taasisi hiyo imeandaa zawadi nzuri kwa washindi watatu wa mwanzo kwa kila kundi zawadi hizo zitasaidia kuwapa hamasa huku washindi watatu watakaoshinda katika riwaya ya Warshi watapewa nyongeza ya zawadi Ili kuwahamasisha zaidi.
Sheikh Zuberi amesema kutakuwa na zawadi Maalumu kwa washiriki wadogo kuliko wate huku mshiriki mdogo atatokea Tanzania pia zawadi kwa kila mshiriki aliyekuja kushindana katika mashindano hayo.
Naye Katibu Mkuu wa Taasisi ya Muhammad VI ya Maulamaa kutoka nchini Morocco Sheikh Mohammed Lafq ameishukuru serikali ya Tanzania na Rais wake Samia Suluhu Hassani kwa mapokezi mazuri waliyoyapata kuruhusu mashindano haya kufanyika nchini .
Sambamba na hayo amesema katika mashindano hayo pia kutakuwa na maonyesho ya Misahafu ya Qurani Tukufu ikiwa na lengo ya kutoa mchango wa kukitunza kitabu cha Allah kwani yataleta historian jinsi Msahafu ulivyokuwa unachapishwa nchini Moroco na namna ya uzuri wake wa kipekee .
“Katika Maonyesho haya Taasisi ya Uongozi wake wa Amirul Muuminiina Mfalme Muhammad VI inaonyesha kwa jinsi gani Falme imeweza kuwatunza na kuwasimamia wote waliokuwa wanahifadhi vema Tamaduni na miiko ya Uandishi wa Msahafu Mtukufu tangu karne na Karne mpaka kufikia hii Leo bado upo” amesema Lafq
Aidha BAKWATA inapenda kuwaalika washiriki wote kuhudhuria na kufuatilia kupitia vyombo vya habari kwani kutakuwa na Semina mbalimbali na mafunzo na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya kuhitimisha.