Home Kitaifa AUA MTOTO WA MIEZI 3 KWA KUMCHOMA KISU,NAE AUWAWA NA WANANCHI WENYE...

AUA MTOTO WA MIEZI 3 KWA KUMCHOMA KISU,NAE AUWAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI

-AMCHOMA PIA MAMA NA BIBI WA MTOTO

  • Na Shomari Binda-Musoma

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Omary Muha mkazi wa Kijiji cha Busekera Musoma vijijini amemua kwa kumchoma kisu mtoto wa miezi 3.

Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo lililotokea jana majira ya mchana ameiambia Mzawa Blog kuwa mtu huyo alianza kumchoma mtoto huyo kisha kumchoma mama wa mtoto na bibi yake.

Amesema mama wa mtoto ni binti wa mke wake aliyekuwa akiishi nae kijijini hapo ambaye hakuzaa nae mtoto huyo.

Shuhuda huyo ameeleza kuwa baada ya kutekeleza tukio hilo mtuhumiwa alijaribu kukimbia na kupigiwa yowe na wananchi kisha kupigwa hadi kupoteza uhai.

Kwa kweli tukio hilo limetokea hapa kijijini na hatujajua sababu zilizopelekea kuchukua uamuzi wa kufanya hivyo.

Muhusika wakati anajaribu kukimbia alipigiwa yowe na wananchi na kupigwa kwenye eneo la uwanja na kupoteza maisha”, amesema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Musoma ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Dk.Khalfan Haule alipofanya mazungumzo na Blog hii amesema yupo Mwanza analifatilia tukio hilo.

Mzawa Blog inaendelea kufatilia tukio hili jeshi la polisi mkoani Mara na kujua hali za majeruhi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!