Home Kitaifa ATIWA HATIANI KWA KOSA LA UBADHILIFU WA FEDHA – RUVUMA

ATIWA HATIANI KWA KOSA LA UBADHILIFU WA FEDHA – RUVUMA

Machi 21, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Nyasa, mbele ya Mh OSMUND NSACKHATU NGATUNGA, imeamliwa kesi ya Rushwa namba 6013/2024.

Kesi hii ni ya Jamhuri dhidi ya Bw. Rainely Mathias Ngonyani ambaye ni katibu wa kikundi cha Walemavu Liparamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Mshitakiwa alishtakiwa kwa kosa la ubadhilifu kinyume na Kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 mapitio ya 2022 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 mapitio ya 2022 kwa kujipatia manufaa tsh. 2,000, 000/= (milioni mbili) fedha za kikundi cha Walemavu Liparamba walizopewa kutoka Akaunti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa kwa ajili ya kina mama, watoto na walemavu na hivyo kufanya upotevu wa kiasi hicho ambacho ni mali ya Halmashauri ya Nyasa.

Kesi iliongozwa na Wakili Mwandamizi Mwinyi Yahaya ambapo mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kukiri kosa lake na kuthibitisha kuwa amesharejesha fedha 2,000,000/- kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa.

Aliomba kupata adhabu nafuu kwa kuwa ni kosa lake la awali na ni mlemavu.

Mahakama imemhukumu mshtakiwa adhabu ya *kulipa faini ya shilingi 100,000/- au kifungo cha miaka miwili jela.

Mshtakiwa amelipa faini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!