Na. Scolastica Msewa, Dar es Salaam
Asilimia 90 ya Wastaafu nchini hupoteza fedha zao za mafao kwa sababu ya kuwekeza fedha zao wakiwa hawana elimu ya uwekezaji wa akiba na kuongeza mitaji yao ambao huishia kupata hasara wanapowekeza fedha zao za mafao.
Hayo yamesemwa na Afisa Masoko wa UTT Bi Dorice Mlenge ambaye ni mmoja wa watoa mada katika kongamano ya Women Ubuntu Tanzania lililoandaliwa na Mkurugenzi wa umoja wa wanawake Washereheshaji/Wajasiriamali Tanzania Dkt. Angella Gloria Bondo.
Dorice alisema wafanyabiashara na wafanyakazi vijana waanze kuwekeza akiba kadri wanavyopata ili iwasaidie kupata uzoefu na wajue chakuwekeza badala ya kuwekeza fedha zao uzeeni wakaishia hasara kwa sababu ya kuwekeza bila uzoefu na bila elimu ya uwekezaji.
Alisema anapenda kuwashauri Watanzania waweke akiba kwani kwa jinsi ambavyo Watanzania wengi hawajapata uelewe kuhusu uwekezaji akiba.
Alisema wengi huamini wanaoweza kuweka akiba ni wale wenye kiwango kikubwa cha fedha au mpaka apate fedha nyingi ndipo aweze kuweka akiba dhana ambayo sio kweli kwani mwenye kiwango kidogo anauwezo wa kuweka akiba ili uweze kuongeza kipato chake pia.
Alifafanua kuwa elimu hiyo uwekaji wa akiba imeweza kuwa changamoto hasa kwa Wastaafu ambao asilimia 90 ya Wastaafu Kila mwaka hupoteza fedha zao kwasababu hawakuweza kujifunza jinsi ya kuwekeza fedha zao.
Aidha ameomba wenye uelewa wa uwekezaji wa akiba waelewesha wenzao kuweka akiba kwaajili ya maisha yao ya baadae ili wakati wa uzeeni tuweze kuwa tumekwishajipanga tayari namna gani ya maisha kwani fedha zinapotea kuwekeza uzeeni.
“Fedha zinapotea wakati wa ujana tukiamini tutapata lakini mwisho wa siku huishia kuishi katika mazingira duni” amesema Dorice.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kuwajengea uwezo Wanawake wafanyabiashara na Ma-MC Dkt. Angela Bondo amesema ni mwaka wa nne Sasa amekuwa akiwakusanya Wanawake na kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli zao ili wapate tija katika jitihada zao za Kila siku.
Alisema alichofanya lengo ni kuwajengea uwezo ili wafanye shughuli zao ili waje kuwa Wanawake bora kwenye unenaji mzuri kwani bila kupata elimu hawawezi kufanya kazi katika ubora uliokusudiwa.
Alisema katika kongamano hilo Wanawake wamejengewa uwezo kuhusu kutangaza biashara zao ili waweze kunadi vizuri biashara zao, jinsi ya kuwa mjasiriamali hodari na kufanyiwa maombi ili Wanawake wawe na nguvu ya kiroho bila kujali dini wala dhehebu la mtu.