Home Kitaifa APRM; SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAJITAHIDI KUTATUA KERO ZA WANANCHI

APRM; SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAJITAHIDI KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Na Magrethy Katengu

Katibu Mtendaji APRM Tanzania Mpango wa hiari wa nchi za umoja wa Afrika kujipima kwa vigezo vya Utawala bora Lamau Mpolo amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan serikali imejitahidi kutatua kero za wananchi ikiwemo kusambaza huduma za maji, umeme, miundombinu, hospitali, shule

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati alipotembelea maonyesho ya sabasaba katika banda la APRM ambapo amesema Tanzania kama mwanachama imekuwa ikipimwa kwa vigezo vilivyowekwa na tafiti hukusanywa kupitia maoni ya wananchi wanayotoa wenyewe na kubaini kuwa Tanzania inapiga hatua katika kutatua kero za wananchi.

APRM Makao yake makuu yapo Afrika kusini na kila mwananchi mwanachama ambaye ameridhia kujiunga ana ofisi hivyo Tanzania iliridhia kujiunga mwaka 2004 na 2006 walianza shughulia zao za utafiti na Ofisi yake iko chini ya Wizara ya Mambo ya nje na Afrika Mashariki ikiratibu masula ikiwemo siasa,maendeleo ya kiuchumi na usimamizi wake,utawala bora ” amesema Lamau

Sambamba na hayo amesema wamekuwa wakibadilishana uzoefu nchi na nchi kwa kutathimini utendaji wa nchi na nchi kujifunza mazuri ikiwemo masuala siasa, Utawala bora,maendeleo ya uchumi na usimamizi wake na wamepanga kufanya tathimini ya nchi zote na kutoa ripoti mbele ya wakuu wa nchi

Amesema Serikali ya awamu ya sita katika tafiti zao walizofanya wameona kuna mabadiliko makubwa katika sekta binafsi kuwabadilishia baadhi ya sera na kusaidia kuvutia wawekezaji kuja Tanzania

Sanjari na hayo amesema Tanzania kulikuwa kero za Muungano zaidi ya 20 lakini APRM imesadia zimetatuliwa na kubakia kero 3 kwa kutoa tafiti zao pamoja na maoni kutoka kwa wananchi.

Aidha APRM imekuwa ikishirikiana wadau mbalimbali ikiwemo REPOA,Chuo kikuu cha Dar es salaam watafiti wengine kufanya tafiti na kutoa ripoti zao na ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda hilo kuuliza maswali na kutoa maoni yao serikali iwafanyie

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!