Home Kitaifa AOMBA KUMUONA RAIS, KUELEZA CHANGAMOTO ALIZONAZO

AOMBA KUMUONA RAIS, KUELEZA CHANGAMOTO ALIZONAZO

Na Neema Kandoro Mwanza

MJASIRIAMALI mwenye matatizo ya ulemavu wa viungo vya mwili ameomba taasisi zinazohusika kumwezesha fursa ya kumwona Rais Samia Suluhu Hassan Ili aweze kumwelezea changamoto zinazomkabili.

Rai hiyo imetolewa Leo Jijini Mwanza na Suki Pirbhai Craft ambaye hawezi kusimama na kutembea katika Maonesho ya kibiashara kwa bidhaa toka nchini Syria ambayo imeanza katika eneo hili na kutarajiwa kufikia tamati Disemba 4.

Alisema anaiomba serikali ya awamu ya sita kumsaidia ili aweze kuongeza mtaji na kukuza mradi wake na hivyo kuweza kuleta maendeleo kwenye kazi zake..

Suki alisema kutokana na hali yake ilivyo imekuwa ni changamoto kubwa kukabiliana na ushindani kutoka kwa wafanyabiashara ambao ni wazima ambao wana uwezo wa kuwafikia watu wa aina mbalimbali.

Mmoja wa wajasirimali huyo Suki Pirbhai Craft ambaye anajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za asili ya kiafrika mshindi kwenye Maonesho ya Afrika Mashariki aliomba kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan a Ili amweleze changamoto zinazomkabili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!