Home Kitaifa ALIYETAMBULIWA KUWA MFANYAKAZI BORA BUKOBA AIPONGEZA SERIKALI NA CHAKUHAWATA

ALIYETAMBULIWA KUWA MFANYAKAZI BORA BUKOBA AIPONGEZA SERIKALI NA CHAKUHAWATA

Na Theophilida Felician Kagera.

Mwalimu wa shule ya Sekondari Rwamishenye Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Japhari Mohamedi Omari aliyefanikiwa kutunukiwa tuzo ya mfanyakazi bora kwenye maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi 2024 ametoa pongezi na shukrani kwa serikali kupitia mwajiri wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba pamoja na chama cha kulinda na kutetea haki za walimu nchini CHAKUHAWATA.

Mwalimu huyo alieleza hili jana Tarehe 3 Mei 2024 baada ya kupokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa chama Manispaa ya Bukoba katika Ofisi ya chama iliyopo kata Kashai.

Amesema kwamba tuzo hiyo ni juhudi zake kwakushirikiana nawenzake kazini jambo ambalo limepelekea kumuibua mfanyakazi bora kati ya walimu saba waliobahatika kupata tuzo hizo kutoka chama hicho.

Sifa zilizompelekea mwalimu huyo kutambuliwa katika ubora huo nipamoja na ufaulu mzuri katika somo la kiingereza kwa kidato channe, kusimamia vyema mazingira ya shule, na usimamizi mzuri wa ujenzi wa miradi ya miundombinu ya shule ambapo miradi ilikamilika kwa ubora.

“Kwenye shule yangu nimetoka mimi pekee mfanyakazi bora na mkuu wa shule ameona jitihada, maafisa elimu kata wameona jitihada hata afisa elimu sekondari wilaya ameona kwamba nafaa katwaa hii nafasi yakuwa mtumishi bora kwa manispaa ya Bukoba” ameeleza mwalimu Japhari.

“Nawapongeza viongozi wa chama changu cha CHAKUHAWATA ngazi ya wilaya na taifa kwani pamoja na mimi kuchaguliwa na mwajiri nikapewa zawadi ya Sh laki 500,000 pia chama nao wakaniandalia zawadi ya cheti nakunikabidhi hii leo nawashuruni sana sana” Japhari.

Hata hivyo ameahidi kuongeza bidii katika majukumu yake ili kuendelea kuwa mfanyakazi mahiri.

Ametoa wito akiwasihi walimu kujituma katika uajibikaji ili kuyavuna mafanikio kede kede huku akiwakaribisha kujiunga na CHAKUHAWATA maana ni chama kilichosimama vyema katika utendaji kazi wake na hiyo imekipelekea kiwatoa wafanyakazi walio bora kwa kasi kama ilivyojitokeza kwake yeye.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHAKUHAWATA Aidani Mganyizi Gerald pamoja naye Katibu wachama Edgar Nambunga baada ya kumkabidhi cheti ameyabainisha baadhi ya masuala ambapo awali ameanza kuelezea mkutadha wa chama zaidi ikiwa kulinda nakutetea haki za walimu.

Amesema kuwa chama hicho kilianzishwa mwaka 2015 nia ikiwa ni kudumisha mahusiano mema kazini, kuongeza utetezi zaidi kwa masuala ya walimu hivyo kimepiga hatua yakuwa na wanachama 587 kati ya zaidi ya walimu 800 walipo Manispaa ya Bukoba.

Ameendelea kufafanua kwamba kutokana na juhudi za utendaji kazi wa chama kimekubalika kwa walimu walio wengi licha yakuwepo kwa vyama vingine kwani kinaaminiwa katika kuhimiza uchapakazi, kukemea migogoro katika vituo vya kazi na mengineyo.

Mwenyekiti Aidani amewapongeza walimu saba kati ya kumi bora waliofanikiwa kutunukiwa tuzo kupitia chama hicho na serikali kwa ujumla.

“Wanachama wetu saba wamepata tuzo ya wafanyakazi bora akiwemo huyu Japhari ambaye ameibuka na ufaulu mzuri wa wanafunzi wa kidato cha nne kupitia soma la Kiingereza hilo siyo jambo jepesi nijambo linalotokana na hamasa zetu sisi tunawatetea iwapo mmepata matatizo kazini, lakini ni lazima muhakikishe mnafanya kazi yenu vizuri ili hata mwajiri alidhike hata kama tunaiambia serikali kwamba watu hawa wanahitaji nyongeza ya mshahara ionekane tija ipo” Mwenyekiti akieleza kwaupana.

Aidha amegusia uwepo changamoto yakutokuwepo kwa mawasiliano ya karibu kati ya chama na waajiri katika masuala yanayokuwa yakiwahusu wafanyakazi hali ambayo imechangia kujitokeza kwa changamoto kadhaa kwa wafanyakazi.

Ametolea mfano taratibu na miongozo ya uhamisho huelezea mfanyakazi akitaka kuhamishwa lazima siku 14 kabla yakuambiwa alipoti kituo cha kazi tayari awe amepewa posho yakujikimu jambo ambalo limekuwa halitekelezeki kwa wakati, wakati mwingine hutolewa kwa kuchelewa huku akilitaja na suala la mishahara midogo.

Amewasihi walimu kujiwahi na kujiunga na chama hicho kwa makato ya Sh 5000 kwa kila mwezi kwani ni chama kilichosimama imara na malengo dhabiti katika kuwa saidia walimu.

Hata hivyo ameipongeza serikali kwakufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu kwakufanyia malekebisho ya ubora mambo kadhaa ikiwemo ya mafunzo kazini, kuimalika kwa mahusiano ya wafanyakazi na waajiri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!