Home Afya AKINA MAMA WAHIMIZWA KUWANYONYESHA MAZIWA YA MAMA PEKEE WATOTO KWA MIEZI 6...

AKINA MAMA WAHIMIZWA KUWANYONYESHA MAZIWA YA MAMA PEKEE WATOTO KWA MIEZI 6 TANGU KUZALIWA

Na Theophilida Felician, Kagera

Wazazi hususani akina mama Mkoani Kagera wemekumbushwa na kuhimizwa kuwanyonyesha maziwa ya mama pekee watoto wao kwa kipindi cha miezi (6) tangu wanapozaliwa hadi kufikia muda huo

Akielezea hayo Afisa lishe wa Mkoa Kagera Joanitha Jovin wakati akizungumza na Blog hii ofisini kwake katika Hospatali ya Rufaa ya Mkoa Kagera Bukoba Manispaa ya Bukoba amesema kuwa mtoto akipatiwa haki yake yakunyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila ya kupewa kitu chochote inamsaidia kumjenga na kumlinda kiafya hatimaye kuepuka madhara ya magonjwa ya ina mbalimbali na tatizo la udumavu na utapiamlo.

Amefafanua kuwa Serikali inasisitiza suala la unyonyeshaji kwa sababu kuna mwingiliano mkubwa kati ya maendelo ya ukuaji wa mtoto na unyonyeshaji kwani mtoto aliyenyonya vizuri na ambaye hajanyonya vizuri huwa tofauti.

Hakuna chakula dunia chenye virutubisho vyote vya kutosha vinayohitajika kwa mtoto wa chini ya miezi 6 zaidi ya maziwa ya mama ndo maana wamama wanasisitizwa zaidi waweze kuwanyonyesha watoto miezi hiyo ya mwanzo maana ni faida kiafya hata kwa mama kwani pale mwanzoni mtoto anapoanza kunyonya inamsaidia kurudisha tumbo la uzazi kwa wakati, sambamba na kuepusha salatani ya matiti na mengineyo” amesema Joanitha Jovin.

Amezitaja baadhi ya faida za unyonyeshaji kwa watoto moja wapo nikumjengea kinga imara ya mwili itakayomwezesha na kumsaidia kutoshambuliwa na magonjwa yakiwemo ya kuhalisha kama atakuwa amepewa vyakula kabla ya kutimia kwa kipindi hicho cha miezi( 6)

Hata hivyo ameleeza kwamba baadhi ya wazazi wamekuwa wakishindwa kutimiza wajibu wakuwanyonyesha maziwa badala yake huwapatia vitu vingine hasa hasa ujiji.

“Wazazi wengi wamekuwa wakiwaanzishia uji watoto kabla ya muda husika mtoto kila anapolia anapewa uji kila anapo lia anapewa uji mtoto hahitaji mahindi wala hahitaji ulezi peke yake anahitaji matunda, mbonga za majani, mayai na maziwa mtoto anahitaji makundi nane ya vyakula vyenye lishe bora” ameendelea kutoa ufafanuzi Afisa Joanitha.

Aidha ametoa wito juu ya kuzingatia muda wa kunyonyesha angalau kwa muda wa dakika 30 kwa titi moja ili mtoto apate kunufaika vizuri na maziwa hayo ya mama iwe kunyonya moja kwa moja kifuani ama yaliyokamuliwa hivyo mtoto anapotimiza miezi hiyo sita anapewa vyakula tofauti tofauti huku akiendelea kunyonya hadi umri wa miaka( 2) unaokubalika kitalaamu wa kumwachisha maziwa ya mama.

Afisa huyo amesisitiza kwamba suala hilo likizingatiwa ipasavyo na jamii pia litasaidia kupunguza kiwango cha udumavu na utapiamlo kwa watoto Kagera ambapo ametoa pongenzi nakuyashukuru mashirika mbalimbali yanayoshirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi kadha wa kadha ya afua mbalimbali za lishe Mkoani humo.

Abimeleck Richard kutoka Shirika linalotekeleza mradi wa mtoto kwanza ambalo siyo lakiserikali (TADEPA) nao wakiwa wameibeba agenda ya unyonyeshaji katika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujua umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama pekee na jinsi inavyowasaidia kukua vizuri watoto kiafya na kielimu.

Amesema kuwa wiki ya unyonyeshaji ni wiki ya kuwahamasisha na kuwakumbusha wazazi kuzingatia sauala hilo kwani ni endelevu na lakudumu.

Richard pia ameongeza kuwa katika mradi wanaoutekeleza wa mtoto kwanza wenye maeneo matano ambayo ni afya, ulinzi na usalama wa mtoto, lishe na elimu ya awali sambamba na malezi mazuri kwa mtoto umejumuisha mambo yote hayo kwa malengo yakuhakikisha mtoto anapata haki za msingi kama hizo bila ya kuacha nyuma zaoezi muhimu la unyonyeshaji.

Ikumbukwe kuwa kila tarehe 1/ 8 hadi 7/ 8 kila mwaka duniani kote huadhimisha wiki ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!