Home Kitaifa AKINA MAMA KAGERA WAHIMIZWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU MALEZI BORA YA WATOTO.

AKINA MAMA KAGERA WAHIMIZWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU MALEZI BORA YA WATOTO.

Theophilida Felician Kagera.

Mwenyeki wa jukwaa la wanawake Wilaya Ngara Christina Mapunda amewakumbushia akina mama umuhimu wa kuwalea watoto kwa kuzingatia misingi ya malezi yaliyo bora ili kuwasaidia watoto hao kukua katika makuzi mazuri.

Mwenyekiti Christina pia akiwa makamu Mwenyekiti wa jukwaa hilo ngazi ya Mkoa ametoa wito huo akiwasilisha mada ya Maisha ya Ndoa kwenye tamasha la umoja wa kikundi cha Kagera Women Galla lililofanyika wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.

Amefafanua kuwa wanawake wengi kwa sasa wamekuwa wakilichukulia kawaida sana suala la malezi bora kwa watoto hali ambayo imekuwa nichangamoto kubwa kwa maisha ya watoto ya kila siku.

“Tumemuomba Mungu atufundishe jinsi ya kuwalea hawa watoto tulio pewa? tuna watoto tunaowalea pengine wamepata ulemavu hawezi kutembea, kuna mtu alimnyanyapaa mtoto wake wakumzaa mwenyewe mpaka anafariki ndani mama hajui mtoto wanakuja kuangalia maiti yake imekakamaa haiwezi kunyooshwa ni mtoto wake inauma naludia tunawaleaje? hebu niwaulize akina mama wenzangu tunamuda wakukaa na watoto wetu? tunamuda wakuongea nao? au tuko na heka heka za biashara weeee! ukiamka saa kumi na moja aljafajiri mpaka saa kumi na mbili jioni ndo unaludi, haya unatafuta pesa ili uje kula na nani?” ameeleza bayana Mwenyekiti Christina Mapunda.

Ameendelea kufafanua kwamba watoto wengi wanapotea, wanabakwa wanalawitiwa maana watoto wako huru mno wanajiongoza kutokana na akina mama kujikita kwenye majukumu ya hapa na pale katika utafutaji kipato.

“Ngoja niwaache na swali hili akina mama pamoja na utafutaji wetu tuangalie na uzao huu Mungu alioutupa tutadaiwa tutatoa hesabu tutafute kwa hakili lakini angalia na uzao wako unauleaje, kuna kuzeheka kuna kuishiwa nguvu nani atakuhudumia? nani atakuletea maji? ndo utaanza kulaani kila mtu” ameendelea kusisitiza wazi mbele ya wanawake Christina Mapunda.

Ametoa baadhi ya mifano yamalezi yanayotakiwa kwa mtoto wakike na kiume ni pamoja na kuwapatia elimu bora, kuwajengea uwezo wa kufanyakazi za ina mbalimbali katika familia kuwalea kwakuzingatia msingi ya maadili ya kumtii Mwenyezi Mungu na mengine mengi.

Jambo kubwa alilolisisitiza ni kwamba kila mtu hususani wanawake wanawajibu mkubwa kwenye ndoa wakushiriki ipasavyo katika kuwalea watoto maana mama ni kiongozi kwa mambo yaliyo mengi katika familia.

Hata hivyo amekemea vikali baadhi ya akina mama wanaowabagua na kuwanyanyasa watoto hasa wale wenye wadada wakazi majumbani jambo ambalo halifai katika jamii.

Amehitimisha akisema kuwa mtoto aliyelelewa katika malezi na makuzi bora anakuwa mama bora na baba bora katika maisha ya ndoa yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!