
Na Magrethy Katengu – Mzawa Media
Dar es salaam
WATEJA sita wa Akiba Commercial Bank Plc kutoka matawi mbalimbali wametunukiwa zawadi za fedha taslimu pamoja na zawadi nyingine, baada ya kuibuka washindi wa kampeni ya Twende Kidijitali – Tukuvushe Januari.
Akizungumza Februari 2025 wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Afisa Biashara Mkuu wa Akiba Commercial Bank, Bi Wezi Olivia Mwazani, amesema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwahamasisha wateja wa benki kutumia huduma za kidijitali kwa urahisi zaidi, kwa kuwa zinaboreshwa pia upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongeza usalama wa miamala.
Washindi hao walipatikana kwa kuangalia matumizi yao makubwa ya huduma za kidijitali, zikiwemo ACB Mobile, Internet Banking, na VISA card hivyo amewapongeza washindi na kuwashukuru kwa kushiriki katika kampeni hiyo na waendelee .

“Tunawapongeza washindi wetu kwa kuwa sehemu ya safari yetu ya kidijitali. Kupitia huduma kama ACB Mobile, Internet Banking, na VISA card, wateja wetu mmeweza kufanya miamala kwa haraka, ikiwa na usalama na kwa urahisi zaidi tunawahamasisha wengine kuendelea kutumia huduma hizi kwa manufaa yao,” alisema Bi Wezi.
Baadhi ya washindi wa kampeni hiyo walieleza kufurahishwa na hatua ya benki kutambua matumizi yao ya huduma za kidijitali kwa zawadi na hamasa hivyo wamepata uzoefu mzuri wa kutumia huduma hizo na wataendelea kuzitumia kwa sababu ya urahisi wake.
Kampeni ya Twende Kidijitali – Tukuvushe Januari ni sehemu ya mkakati wa Akiba Commercial Bank wa kuhamasisha matumizi ya huduma za kidijitali ili kuwapatia wateja wake suluhisho bora na la kisasa katika upatikanaji wa huduma za kibenki popote walipo.
