Home Kitaifa AFYA YA UDONGO KUPIMWA VIJIJI 100 MKOA WA MARA NA SERIKALI KUPITIA...

AFYA YA UDONGO KUPIMWA VIJIJI 100 MKOA WA MARA NA SERIKALI KUPITIA OCP AFRIKA

Na Shomari Binda-Musoma

JUMLA ya vijiji 100 vilivyopo mkoani Mara,vinatarajiwa kufikiwa katika zoezi la upimaji wa afya ya udongo ili kupata mazao yenye tija.

Zoezi hilo litakalofanywa na serikali kupitia kampuni ya OCP Afrika limetajwa kuwa mkombozi wa kumuinua mkulima na kuwa na mazao yenye manufaa.

Akizungumza kwenye kikao kazi kilichowashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wakulima,mkurugenzi wa Tari, Denis Tipe ,amesema upimaji wa afya ya udongo na tathimini yake ni jambo la muhimu ambalo linakwenda kuinua kilimo.

Amesema usipojua afya ya udongo na tathimini yake huwezi kupata kilimo chenye manufaa ambacho na kuachana na kilimo duni

Mkurugenzi huyo amesema vijiji 100 vitakavyofikiwa na mradi huo vitasaidia kufikia malengo ya kujua afya ya udongo kwa mkoa wa Mara.

Katika hotuba ya mkuu wa mkoa wa Mara,Saidi Mtanda, iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Serengeti,Vincent Mashinji,amesema zoezi hilo limekuja wakati muafaka.

Amesema serikali kwa sasa inakwenda kuwekeza zaidi kwenye kilimo hivyo lszima kuw na udongo unaofaa kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Kwenye hotuba yake amesema hali ya uvunaji wa mazao kwa mkoa wa Mara imekuwa chini hivyo zoezi la upimaji wa afya ya udongo inakwenda kusaidia wakulima.

” Tunaishukuru serikali kwa kuleta zoezi hili la upimaji wa afya ya udongo na tathimini yake ambsyo inakwenda kusaidia kilimo chetu cha mkoa wa Mara”,amesema.

Baadhi ya washiriki wa zoezi hilo la upimaji wa udongo utassidia kwa kiasi kikubwa kupata kilimo.chenye tija na kuishukuru serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwa kukusudia kuinua kilimo hapa chini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!