Home Kitaifa ADC KUTAFUTA MRITHI WA MWENYEKITI WA ADC HAMAD RASHID MFAUME

ADC KUTAFUTA MRITHI WA MWENYEKITI WA ADC HAMAD RASHID MFAUME

Na Magrethy Katengu

Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo ametangaza dhamira ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Taifa baada ya Hamad Rashid Mohammed kumaliza muda wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 6, 2024 jijini Dar es Salaam, Doyo amesema ametangaza rasmi kuwania nafasi hiyo kwa kuamini ana uwezo wa kukitumikia chama hicho katika kutekeleza matakwa ya Katiba ya chama hiko

“Mimi nimejipanga kuwa mwenyekiti wa chama hiki ili kurithi mikoba ya Mheshimiwa Hamadi Rashid kwa sababu nimepata mafunzo makubwa sana hekima na busara kutoka kwake kwani huyu ni mwanasiasa mzoefu na amefanya kazi na wanasiasa wakongwe miaka mingi amesema Doyo.

Doyo amefafanua kuwa Hamad amewafunza mambo mengi wanachama kwani ameonyesha mfano wa kuigwa kutong’ ang’ania uenyekiti amefuata matakwa ya Katiba kwa kuachia ngazi baada ya kumaliza muda wake hivyo ni funzo kubwa kwa vijana wa chama hicho na wana siasa wengine nchini.

Doyo ameeleza kuwa kati ya mafunzo aliyopata kutoka kwa mwanasiasa huyo mkongwe ni uvumilivu , ustahimilivu hekima na busara katika kupambana na kila changamoto za kisiasa

Aidha wanachama wote wanahaki kisheria kuwania nafasi hiyo pia amemkaribisha Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema kujiunga na chama hicho endapo haridhishwi na mambo yanavyokwenda huko aliko CHADEMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!