Home Michezo ADAM ADAM AREJEA AZAM FC

ADAM ADAM AREJEA AZAM FC

Klabu ya soka ya Azam FC imeamua kumrejesha nyota wao wa zamani, Adam Adam, kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja. Adam Adam, ambaye msimu uliopita alikuwa na timu ya Mashujaa FC ya Kigoma, sasa anarejea kwenye klabu aliyoanza nayo soka la ushindani.

Adam Adam ni zao la akademi ya Azam FC, ambapo alikuzwa na klabu hiyo kuanzia mwaka 2011 mpaka 2014. Hii ina maana kuwa, ni takribani miaka 10 imepita tangu nyota huyo aondoke Chamazi. Kurudi kwa Adam Adam katika viunga vya Azam Complex kunatarajiwa kuongeza nguvu na uzoefu kwa timu hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!