Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameunda Kamati ya Kuunda Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2025, ambapo amefanya uteuzi wa wajumbe 12 pamoja na sekretarieti 4.
Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kiongozi wa Chama hicho, tarehe 6 Februari 2025, jijini Dar es Salaam, Emmanuel Lazarus Mvula ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, huku Idrisa Kweweta akiteuliwa kuwa Katibu wa Kamati.
Emmanuel Mvula:
Mvula amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sera na Utafiti Taifa (2016-2019), Mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT Wazalendo (2019-2024), na pia Mjumbe wa Kamati ya Maadili Taifa (2024 – hadi sasa). Aidha, amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Ushindi Taifa (2020) katika Kampeni za Chama. Mvula pia alikua Mjumbe wa Kamati ya Kuandaa Ilani ya Uchaguzi ya 2015-2020 na Mjumbe wa Kamati Kuu 2020-2024.
Idrisa Kweweta:
Kweweta amewahi kuwa Katibu wa Kamati ya Sera na Utafiti Taifa (2016-2019) na pia Katibu wa Sera, Utafiti na Mafunzo Taifa (2019-2024). Amefanya kazi kama Meneja wa Mafunzo katika Timu ya Ushindi ya Taifa (2020) na Mratibu wa Tafiti za Uchaguzi (2016-2024). Alikuwa Mkuu wa Sera na Utafiti katika Baraza Kivuli la Mawaziri (2022-2023), na Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza Kivuli la Mawaziri la ACT Wazalendo (2023).
WAJUMBE WA KAMATI |
|
---|---|
Dkt. Elizabeth Sanga |
Abdul Nondo |
Prof. Omar Fakih |
Yasinta Cornell Awiti |
Mary Mongi |
Seif Suleiman Hamad |
Mtutura Abdallah Mtutura |
Shangwe Ayo |
Pavu Abdallah |
Humphrey Mrema |
Edgar Mkosamali |
Maharagande Mbarala |
SEKRETARIETI YA KAMATI |
|
---|---|
Mshenga Juma |
Jackline Prosper Ndonde |
Jasper Sabuni |
Said Mahalifa |