Home Kitaifa ACT-WAZALENDO IMEITAKA SERIKALI KUHAKIKISHA INASIMAMIA MASLAHI YA WAONGOZA WATALII

ACT-WAZALENDO IMEITAKA SERIKALI KUHAKIKISHA INASIMAMIA MASLAHI YA WAONGOZA WATALII

CHAMA cha ACT-WAZALENDO kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya waongoza watalii nchini.

Hayo yamesemwa leo tarehe 26 Aprili 2024, na Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Semu alipokuwa akiwaongoza viogozi wengine wa chama hicho alioambatana nao katika ziara ya ‘Utalii wa Kisiasa’ waliotembelea kivutio cha Materuni (Materuni Waterfall) ambapo sasa hawalipwi kinachostahili.

Dorothy amesema kuwa kiwango wanachostahili kulipwa waongoza watalii hao ni Dola 20 za kimarekani lakini kwa sasa wanalipwa kiasi cha Dola 13 mpaka 11 .

Tumezungumza na vijana wanaoongoza watalii wanasema kuwa wanastahili kulipwa kiasi cha dola 20 lakini wanalipa 13 muda mwengine mpaka 11. Tunataka vijana hawa waboreshewe ujira wao ili kuboresha maisha yao” amesema Dorothy.

Dorothy amesema kuwa chama hicho kimeamua kufanya utalii huo ili kujionea hali halisi ili kuendelea kupigania sekta ya utalii kwa maslahi mapana ya taifa.

Amesema kuwa mbali na hayo ameitaka serikali kuboresha mazingira ya utalii hususan vifaa vya uokoaji, na vitendea kazi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa ACT-WAZALENDO Bara Isihaka Mchinjita amesema kuwa Tanzania inapaswa kutumia vizuri fursa kuwa na vivutio vingi vya utalii kuzidisha pato la taifa kwa kuingiza pesa za kigeni.

Zipo nchi zinavivutio vichache vya utalii lakini wanaingiza pesa nyingi za kigeni kutushinda sisi wenye vivutio vingi vya utalii

Naye Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT-Wazalendo Abdul Nondo amesema kuwa waongoza watalii ni vijana hivyo kuna umuhimu wa serikali kuboresha mazingira yao ya kazi.

Vijana wameamua kujiajiri wenyewe kwenye sekta ya utalii hivyo serikali muhimu ikawaboreshea mazingira yao kwa mfano hapa hakuna vyoo watalii wanalazimika kujisaidia vichakani jambo ambalo linafachafua mazingira” alisema Nondo.

Viongozi wa ACT Wazalendo wapo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Demokrasia itakayofanywa tarehe 27 Aprili 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!