
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa na Makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Othman Masoud, amesema kuwa Halmashauri Kuu ya chama hicho imeamua kubadilisha mwelekeo wa siasa na kuanzisha njia mpya ya kufanya siasa ili kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
Masoud amezungumza hayo wakati wa Kongamano la Viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika Machi 12, 2025, katika makao makuu ya chama hicho. Amesema chama kitashirikiana na vyama vyote makini kuhakikisha wanapambania demokrasia na kuwaomba viongozi wa ngazi zote kushirikiana kwa lengo la kuleta mabadiliko katika taifa.

Masoud amesema kuwa anaamini kuwa Tanzania ni tajiri zaidi barani Afrika kwa rasilimali zake, lakini utajiri huo hauwanufaishi wananchi wote. Aliongeza kuwa nchi inahitaji uongozi bora ili kuhakikisha wananchi wanafaidika na rasilimali zilizopo.
“watu hawaibiwi kwa sababu ya uzembe, bali ni kwa sababu ya watu ambao wamezoea kuiba. Alisema kama ingekuwa ni uzembe, basi watu wasingeibiwa hata nyumba za ibada”. Alisema Masoud
Aidha Masoud amesema kuwa CCM haikusherehekea ushindi kwa sababu walishangazwa na matokeo hayo, kwani hawakuupanga, hawakuutarajia, wala hawakuupambana kwa ajili ya ushindi huo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjinjita, amebainisha Sababu ya chama hicho kutoshirishiki katika baraza la vyama vya siasa ni hadi pale masuala muhimu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa yatakapojibiwa. Mchinjinjita alitaja masuala hayo kuwa ni wizi wa kura, kuenguliwa kwa watu, na polisi kuingilia uchaguzi.
Mchinjinjita aliongeza kuwa gharama za uchaguzi wa serikali za mitaa haziwezi kuwa za wananchi pekee, na kwamba kila mmoja anapaswa kugawana maumivu ya uchaguzi uliofanyika