Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro(mwenye shati yenye madoa meupe na meusi), ametembelea katika moja ya mabanda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na kupata elimu ya huduma zinazotolewa na BRELA, katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa, yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa, wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam. Mabanda ya BRELA yapo ndani ya Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara na nje ya Wizara ya Fedha na Mipango.