Na Magrethy Katengu
Makamu Mwenyeki Taifa Chama cha Mapinduzi CCM Abdulrahman Kinana amekishauri Chama cha Upinzani wasiwe watu wa kukosoakosoa tu bali wamfikiria Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani alivyo na Utashi, Makusudi na Nia njema kwa Taifa hili kwani amekuwa msikivu kwa kuwatatulia hoja zao na changamoto zao pale tu alipoingia Madarakani.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaaam katika Mkutano wa Wanachama wa Mkoa wa Dar es salaam Rais hapendi kikundi kimoja kisiwe na furaha hivyo alipoingia tu madarakani alifanya jitihada za Maeidhiano na kurusu mchakato wa katiba mpya na kuruhusu baadhi ya sheria ambazo walikuwa wanazilalamikia kuwa zinawagandamiza hivyo lazima Dkt Rais Samia Suluhu Hassani ieleweke kuwa ni Kiongozi wa upekee.
“Tukumbuke kuwa alipoingia tu Madarakani kulikuwa na wanachama wa Chadema 400 walikuwa Mahabusu kwa sababu za kesi za kiuchaguzi hivyo alitafuta namna ya kuwaachia huru na katika kesi 11 zilizokuwa zikowakabili upinzani zilifutwa 9 na mbili zilishindikana kufutwa na alifanya jitihada za kuwarudisha viongozi wa Chadema waliokimbia nje ya nchi alisihi warudi na aliwahakikishia usalama wao hivyo hebu jifikirieni mmeshawahi kusikia kuna mtu katekwa” amesema Kinana
Sanjari na hayo Kinana amesema pamoja na Dkt Rais Samia Suluhu Hassan kufanya kutumia hekima na busara zake aliporuhusu na mikutano ya kisiasa ya hadhara amekuwa akikejeliwa kutukanwa lakini hajajibu amekuwa mpole na kuchukulia hiyo ni siasa tunaelekea uchaguzi mkuu pia amekubali kujitoa baadhi ya madaraka na kuruhusu tume huru ya uchaguzi .
Hata hivyo Makamu Mwenyekiti Taifa CCM Kinana amesema baada ya Maridhiano kuzungumza nao Viongozi wa Chadema Meza moja walianza kudai ruzuku za kuanzia mwaka mwaka 2021 hadi 2023 hivyo kutokana na Maridhiano walikaa na kuamua kuwalipa bilion zaidi ya bilion 2 hivyo wananchi waangalie jinsi busara na Hekima zaRais Dkt Samia Suluhu Hassani asivyopenda kundi lolote likae na vinyongo.
Aidha pia kuelekea uchaguzi kuanzia ngazi za Serikali za Mtaa mwaka huu na Uchaguzi wa Rais Madiwani na Wabunge mwaka 2025 hivyo kupitia maoni yaliyotolewa kuhusu kuundwa tume huru ya uchaguzi ili kila mtu aridhie.