Home Kitaifa MWAROBAINI WACHEMSHWA KUDHIBITI UPANGAJI NAULI HOLELA MADEREVA TAX

MWAROBAINI WACHEMSHWA KUDHIBITI UPANGAJI NAULI HOLELA MADEREVA TAX

mkurugenzi udhibiti usafiri wa Ardhini Johanes Kahatano
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija katika Ufunguzi Kikao kazi na Madereva tax Mkoa huo kujadili na kutoa maoni namna Mita Tax
Nae kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC), Leo Ngowi amesema
Picha ya pamoja

Na Magrethy Katengu .

Mamlaka ya udhibiti usafiri wa Ardhini (LATRA) imesema kabla ya kufika mwezi Juni mwaka 2023 Wanaosafirisha abiria kwa Tax tayari magari hayo yatakuwa yamefungwa mfumo wa Taxi mita utakasaidia abiria kufahamu kiasi cha nauli anachotakiwa kulipa kulingana na kilometa.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija katika Ufunguzi Kikao kazi na Madereva tax Mkoa huo kujadili na kutoa maoni namna Mita Tax atakavyokuwa na maslagi ya Watumishi tax kuondoa migongano iliyokuwo kati ya dereva na abiria hasa wakati wa kudai nauli hivyo mfumo huo utakavyoanzishwa itamwezesha abiria kutoa kiwango sahihi cha nauli pia mfumo huo utaongeza usalama na uhakika kwa abiria.

“Hivi sasa mfumo unaotumika dereva anamtoza nauli abiria kadri anavyojisikia kwa kuangalia hadhi yake hivyo kwa kutumia taxi mita itawezesha abiria kutoa kiwango cha nauli ambacho ni sahihi na haki na kuepukana na migongano na dereva wakati wa kudai nauli“Mkuu wa Wilaya

Mbali na kulipa nauli sahihi ya uendapo, abiria utakuwa umejiridhisha chombo unachopanda ni chombo ambacho kinatambuliwa na LATRA kwa mujibu wa sheria” Amesema Ludigija.

Kwa upande wake mkurugenzi udhibiti usafiri wa Ardhini Johanes Kahatano amesema LATRA wameitisha kikao hicho na wadau mbalimbali ikiwemo Madereva tax ili kuondoa migongano iliyodumu kwa muda mrefu ili kupitia teknolojia utakavyoanzishwa kila mdau aridhie kusitokee

Kahatano ameongeza kuwa Taxi mita ni mfumo wa uwazi,ukweli na uhakika kwa pande zote mbili yaani Abiri na Dereva kwani kila mtu ataona kiwango halisi cha nauli kulingana na umbali wa sehemu husika.

Nae kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (LATRA CCC), Leo Ngowi amesema Sasa malalamiko kati ya Abiria na Dereva Taxi yameanza kupatiwa mwarobani pia amesema kuna nchi 9 Afrika moja ikiwa ni ya Afrika mashariki ambayo ni Rwanda ambazo zinatumia mfumo wa Tax mita.

Aidha LATRA CCC imetoa mapendekezo matatu ambayo ni Taxi zote zifungwe Taxi mita baadaya mfumo kuanza kazi,kuwe na ukomo wa gari kufungwa taxi mita pia Elimu itolewe kwa Abiria ili wajue uwepo wa Taxi mita na jinsi ya kutumia mfumo huo mpya.

Mwenyekiti wa Shirikishi la Taxi Tanzania Ramadhani Ashiru ameiomba LATRA kufanyiakazi changamoto zilizopo ikiwemo Taxi bubu, bodaboda na bajaji kufanyakazi kiholela ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Taxi mita zinaendana na mazingira yaliypo ya ubovu wa barabara na foleni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!