Home Biashara NMB YAANZISHA UFUNGUAJI AKAUNTI NDANI YA DAKIKA MBILI

NMB YAANZISHA UFUNGUAJI AKAUNTI NDANI YA DAKIKA MBILI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akimsikiliza Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa benki ya NMB, Filbert Mponzi wakati akimueleza juu ya mfumo wa malipo kwa kuskani QR (lipa Mkononi) ya Benki ya NMB katika moja ya Duka lililopo kwenye Stendi ya Mabasi ya Magufuli mara baada ya kuzindua NMB pesa Akaunti ya Benki ya NMB.
Dar es Salaam Regional Commissioner, Amos Makalla listening to the NMB Bank’s Chief of retail banking, Filbert Mponzi on the Bank’s payment method of QR scanning at one of the shops in Magufuli Bus Terminal having launched the NMB pesa Akaunti; a simplified Digital solution of account opening
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Gabriel Makalla (kushoto) akipeperusha bendera pamoja na Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa benki ya NMB, Filbert Mponzi (kulia) wakiashiria kuzindua Rasmi NMB pesa Akaunti katika Stendi ya Mabasi ya Magufuli Jijini Dar es salaam. NMB pesa Akaunti ni mfumo wa kidigitali wa ufunguaji wa akaunti wa benki ya NMB.
Dar es Salaam Regional Commissioner, Amos Makalla(left) waving flags together with the NMB Bank’s Chief of Retail Banking, Filbert Mponzi (right) During the launching of NMB pesa Akaunti; a simplified Digital solution of account opening at the Magufuli bus stand in Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Gabriel Makalla (katikati) akipeperusha bendera pamoja na Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa benki ya NMB, Filbert Mponzi (kulia) wakiashiria kuzindua Rasmi NMB pesa Akaunti katika Stendi ya Mabasi ya Magufuli Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James. NMB pesa Akaunti ni mfumo wa kidigitali wa ufunguaji wa akaunti wa benki ya NMB.
Dar es Salaam Regional Commissioner, Amos Makalla(center) waving flags together with the NMB Bank’s Chief of Retail Banking, Filbert Mponzi (right) During the launching of NMB pesa Akaunti; a simplified Digital solution of account opening at the Magufuli bus stand in Dar es Salaam. Left is the Ubungo District Commissioner, Kheri James.

Na Mwandishi Wetu
Zama mpya ya huduma za kibenki imejiri nchini baada ya Benki ya NMB jana kuzindua suluhisho ya kisasa inayomwezesha mteja kufungua akaunti kidijitali na kuanza kuitumia ndani ya dakika mbili tu.


Hatua hiyo kubwa inaongeza msukumo mpya katika jitihada za taifa za ujumuishwaji wa kifedha na upatikaji kiurahisi wa huduma za kidijitali za fedha.
Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Bw Filbert Mponzi, sifa kubwa ya suluhisho la NMB Pesa Akaunti ni kuwa na mchakato mfupi wa kufungua akaunti mpya.


Hii ni suluhisho yakusaidia kutatua changamoto za kifedha ambayo si tu ni akaunti inafunguliwa hapo hapo mteja alipo lakini pia ni nafuu kwasababu haina gharama nyingi kama ada za mwezi,” Bw Mponzi alisema.


Pia aliiambia hadhara iliyoshuhudia kuzinduliwa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam kuwapindi usajili wa mteja mpya unapokamilika, akaunti yake itafunguliwa mara moja na kuanza kutumika moja kwa moja wakati huo ikiruhusu upatikanaji wa huduma zote za msingi kama ile ya NMB Mkononi.


Moja ya malengo yake makubwa ikiwa ni kuwakwamua Watanzania walio nje ya mfumo rasmi wa kibenki, NMB imeitambulisha sokoni huduma hiyo ya kufungua akauanti kidijitali kwa kasi zaidi nchini kwenye stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Magufuli Bus Terminal.
Bw Mponzi alibwambia ngeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw Amos Makala, kuwa ufunguaji huo mpya wa akaunti unafanyika mahala popote na hauhusishi kabisa karatasi ya aina yoyote na mfunguaji haitaji kwenda wala kufika katika matawi yao 228 yaliyotapakaa nchi nzima.


Jambo hilo limemfurahisha sana kiongozi huyo wa serikali ambaye kwenye hotuba yake aliesma hii sasa ni fursa kwa Watanzania wote kuwa na akaunti ya benki. Ufunguaji huo wa akaunti unafanyika kwa msaada wa wafanyakazi wa mauzo wa benki hiyo kwa njia ya simu za mkononi za aina zote.


Bw Mponzi alisema huduma hiyo itakuwa ya muhimu sana hasa katika maeneo ambayo upatikanaji wa huduma za kifedha bado ni mdogo au haupo kabisa na wenye akaunti za benki ni wachache sana. Kwa sasa NMB inazo akaunti zaidi ya milioni tano na kila ziku zaidi ya 3,000 zinafunguliwa.


Sote ni mashuhuda kuwa ulimwengu sasa unaelekea kuwa wakidigitali kwa karibia kila jambo, na kwa hilo Benki ya NMB imekuwa ikipambana kila mara kuibuka na masuluhisho ya kidigitali ambayo yatazidi kurahisisha utoaji huduma zetu lakini kuzifanya pia ziwe bora zaidi kwa wateja wetu,” alibainisha.


Benki ya NMB imekuwa ikitumia teknolojia kutoa huduma za viwango vya kimataifa kwa wateja wake. Tumeanzisha ufunguaji huu mpya wa akaunti kidijitali ili kukuza zaidi ujumuishwaji na uwezeshaji wa Watanzania ambao bado wako nje ya mfumo rasmi wa kibenki,” kiongozi huyo aliongeza.


Aidha, Bw Mponzi alisema NMB Pesa Akaunti itazidi kupeleka huduma zao karibu na wananchi na kuwawezesha wateja kuhudumiwa kirahisi ikiwemo kuweza kupata mikopo midogo kama ile ya MshikoFasta.
NMB Pesa Account pia itawawezesha wateja kuweka na kutoa pesa kwa NMB Pesa Wakala pamoja na kufanya malipo kwa njia ya LIPA Mkononi.


NMB Pesa ni hatua nyingine muhimu katika safari yetu ya mabadiliko ya kidijitali na inatilia mkazo dhamira ya NMB ya kukuza ujumuishwaji wa wengi kifedha nchini,” Bw Mponzi alisema.


Umairi wa ubunifu wa NMB na uwekezaji wake katika teknolojia mpya umeijengea heshima kubwa nchini benki hiyo na kuifanya itambulike kimataifa. Katika miaka miwili iliyopita pekee, NMB imeweza kujikusanyia zaidi ya tuzo 20 za kimataifa ilizotunukiwa na majarida yanayoheshimika duniani kama vile World Economic Magazine, Global Brands Magazine, International Banker Awards na International Business Magazine.


Bw Mponzi alisema mwaka 2022 ulipoanza lengo la NMB lilikuwa ni kufungua akaunti mpya milioni moja. Mpaka sasa hivi zimefunguliwa 1,012,344


Hii inamaanisha kwa siku mmoja tu NMB tunafungua akaunti mpya 3,135. Hii ndo maana halisi ya huduma za kifedha jumuishi Tanzania,” alifafanua.


Kwa ujio wa NMB Pesa Akaunti bila shaka akaunti nyingine nyingi zitafunguliwa kama ilivyodhihirika jana baada ya Bw Makala kuzindua rasmi msafara wa magari utakaotumika kufanikisha zoezi hilo nchi nzima.
Mkuu huyo wa mkoa alisema benki zipo nyingi nchini lakini zitakazofanikiwa ni kama NMB ambayo kila mara inakuja na ubunifu mpya kusaidia kuwandoelea wananchi karaha na kufanya maisha yao yawe rahisi.


Nimefurahishwa sana na ubunifuu huu wa NMB wa kuja na suluhisho hii. Ni imani yangu sasa idadi ya Watanzania wenye akaunti wataongezeka na hii ni faraja kwa serikali ambayo kiu yake ni kuongezeka kwa watu wanomiliki akaunti za benki nchini,” Bw Makala alibainisha.


Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw Heri James, alisema uzinduzi wa NMB Pesa Akauni ni jambo ambalo litasaidai ustawi wa baishara na uchumi wilayani humo na Tanzania kwa ujumla.
MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!