Na Magreth Mbinga
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Maonyesho makubwa ya sekta ya dawa na huduma za afya East Africa Pharma Healthcare Show ambayo yatahudhuliwa na wadau na wataalamu wa afya kutoka sehemu mbalimbali Duniani.
Hayo yamezungumzwa na Katibu Mtendaji Chama Cha Wanasayansi wa Maabara(MILSAT) Brian Peter Wiliam katika Mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa maonyesho hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam kuanzia Disemba 14 hadi 16 saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni.
“Maonyesho hayo yatawakutanisha wazalishaji,wauzaji wa jumla,wafanyabiashara na wasambazaji wa sekta ya uchunguzi wa dawa,Hospitali na watoa ushauri wenye ushawishi mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki Nchini Tanzania”amesema Brian.
Pia Afisa Wanachama Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Cresensi Mbunda amesema maonyesho hayo yameidhinishwa na Tantrade ikiwa na dhumuni la kutaka Watanzania wapate fursa ya kujifunza, kuimarisha na ushirikianao baina ya Nchi zitakazo shiriki.
“Tunapenda kushukuru mashirika ya Serikali na binafsi yaliyokubali kushirikiana nasi ikiwemo TPSF, TCCIA, CTI, TANEXA, TMDA, TMSA,MAT,MeLSAT, TANHELSO na TWCC”amesema Mbunda.
Aidha Msimamizi wa mradi Thomas James amesema makampuni zaidi ya 90 yatashiriki maonyesho hayo na hakita kuwa kiingilio wananchi wote wanakaribishwa kujifunza na kuona teknolojia ya kisasa katika sekta ya afya kutoka Nchini India.
“Wafanya biashara wa Tanzania watapata fursa ya kukutana na makampuni mengine yanayozalisha vifaa tiba kutoka Nchini India pia Chama Cha wataalamu wa madawa watainyesha fursa za uwekezaji kwa wageni ambazo zinapatikana Nchini “amesema Thomas.