Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TSPF)Imekutana kwa Siku tatu na Wadau mbalimbali wa Sekta Binafsi na Serikali kwenye mdahahalo ulioandaliwa na Taasisi hiyo wenye lengo la kuibua Maoni ambayo yataisaidia Serikali kuongeza Pato la Taifa na Ajira kupitia Uhifadhi wa Maliasili Nchini.
Mdahahalo huo umefanyika Jijini Tanga kwa Siku tatu na kumalizika Leo umelenga kuwaongezea Ufahamu Wadau wa Sekta Binafsi hususani kwenye Sekta ya Uhifadhi na Wanyamapori ambapo Kwa Mkoa wa Tanga umelenga wawekezaji na Wadau wanaotumia pori la Amani ili wafanye shughuli zao bila kuathiri Ushoroba wa Wanyamapori Kati ya Pori la Amani na Niro .
Meneja wa Mradi wa USAIDS Tuhifadhi Maliasili Max Rugaimukamu alisema Mradi huo ni Umefadhiliwa na Watu wa Marekani na umelenga kuongeza Ufahamu kwa Wadau wa Sekta Binafsi juu ya Maliasili Nchini,
“Kwa hapa Mkoa wa Tanga, Mradi huu umelenga kuongeza Ufahamu kwenye Sekta Binafsi juu ya masuala ya Uhifadhi wa Maliasili na Wanyamapori katika maeneo ya mawili ambayo ni Pori la Amani na Niro kwaajili ya Kudumisha Shughuli bila kuathiri Ushoroba wa Wanyamapori Kati ya mapori hayo mawili ambapo Amani Kuna njia za Wanyamapori” Alisisitiza Max
Alisema kwenye mjadala huo Serikali imeshirikishwa kwaajili ya kuyapokea mapendekezo na maoni ya Wadau na Wanaamini Serikali itayafanyia kazi ili kuleta matokeo chanya hususani kwenye Pato la Taifa na Ajira kupitia Uhifadhi wa Maliasili na Wanyamapori,
” Mjadala huu utaendelea Tena Mwakani lakini itakuwa katika ngazi ya Taifa kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii , kwa Sasa maoni na mapendekezo haya tunaamini Serikali itayapokea na kuyafanyia kazi kile ambacho Wadau watakipendekeza kwa lengo la kuboresha Huduma za Maliasili ” Alisema Max
Kwaupande wake Meneja Kambi ya Hifadhi ya Magoroto Mathias Manyanya Alisema Kupitia mdahalo huo wamepata fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabali Sekta ya Uhifadhi,
” Kwa Sisi wahifadhi msitu wa Magoroto ambao ndio Kituo kikubwa Cha Utalii tunapitia changamoto mbalimbali lakini changamoto kubwa inayotukabili ni Uvamizi wa Wananchi kuingia msituni kukata miti na hii inatokana na Elimu ndogo kwa Jamii inayotuzunguka juu ya utunzaji wa Mazingira, Tunaamini kupitia Mjadala huu Serikali itatusaidia kwenye hili” Alisema Mathias
Alisema wameweka utaratibu wa kuzarisha Miche ya miti asili na huwapataia Wananchi Bure kwaajili ya kuongeza Uhifadhi,
” Tumeweka utaratibu maalumu wa kuzarisha Miche kwenye vitalu , Miche hiyo ni miti asili na tunawapatia Wananchi wote wananaoishi vijiji jirani, lengo nikuongeza Uhifadhi, kwenye shughuli zetu tunategemea Viumbe mbalimbali ikiwamo ndege aina ya Hondo Hondo ambao huhama kutoka Amani Hadi Magoroto ambao hutumia msitu kama Hifadhi yao ya makazi na sisi huwapereka Watalii kwenye makazi ya ndege hao pia tuna Viumbe kama vipepeo na Vinyonga hao wote hutegemea Uhifadhi Bora wa Misitu hivyo kupitia Mdahahalo huu utatusaidia kupata suluhu ya kudumu ya Uhifadhi Salama hasa kwa Wananchi wanaotuzunguka kupatiwa Elimu ya utunzaji Rasirimali zao” Alisema Mathias
Mwisho