WAOKAJI wa vitafunwa watakiwa kujisajili ili serikali iwape vipaumbele mbalimbali ikiwemo mikopo ili kupanua biashara pamoja na kupata fursa za kibiashara.
Akizungumza wakati wa kufungua Maonyesho ya biashara na viwanda katika viwanja vya 77 Jijini Dar es salaam Diwani wa Kata ya Mtoni Amina Batashi amesema sekta ya waokaji inaendelea kukuwa kwa kasi zaidi.
“Sekta ya waokaji inazidi kuimarika na kukuwa siku hadi siku kutokana na kundi kubwa ambalo lipo ikijumuisha wanawake na wanaume.
Batashi ameeleza namna serikali imekuwa ikawapa vipaumbele wajasiriamali na wafanyabiashara kwa kuweka Mazingira rafiki ikiwemo mikopo ya mitaji kwa vikundi kwa ajili ya kupanua biashara zao.
Pia amewataka waokaji hao kuhakikisha bidhaa zao zinagusa kila mtu na kuhakikisha anaefika dukani kwake anapata bidhaa zake bila kubaguwa watu wa aina fulani.
“Mtu mwenye kisukari akifika dukani ahakikishe anapata bidhaa zenu,mwenye uzio anapata bidhaa tukifanya hivyo tutakuwa na waokaji wenye ubunifu na viwango vya hali ya juu katika biashara zao kutokana na kujali wateja wote wenye maradhi na wasio na maradhi .
Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara nchini (TANTRADE) Latifa Khamis ametoa rai kwa taasisi za serikali na hata binafsi zinaunga mkono sekta hiyo kwa kupumua bidhaa zao ambazo zina ubora na viwango kuliko kununua bidhaa za kigeni ikiwema biscuit za ofisi na vichangamsha kinywa vingine kwa ajili ya wageni wanaofika maofisini.
Huku akiwataka wajasiriamali hao waouokaji vitafunwa kutumia mitandao ya kijamii kujitangaza biashara zao kwani kwa sasa mitandao ina nafasi kubwa katika kuhakikisha unapata wateja wengi kuliko kusubiri wateja wa dukani ama nyumbani.
“Lazima mfanyabiashara yoyote yule uwe unatumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zako hivyo niwaombe mjiunge ili kutanua masoko yenu ya biashara zenu pia iwe rahisi kupatikana kwenu .“
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha waokaji nchini (TBA) Fransica Rema ameongeza kuwa chama hicho kimepata fursa mbalimbali ikiwemo kufanya semina 2 zilizofanikishwa na Mamlaka ya Maendeleo ya biashara nchini (TANTRADE) na kuleta manufaa makubwa na hatimae waokaji kutengeneza bidhaa zao kwenye viwango na kuhakikisha bidhaa hizo zina vifungashio vyenye ubora zaidi.
Hata hivyo Lema ameeleza kuwa chama hicho kinaendelea kukuwa siku hadi siku kutokana na sekta ya uokaji kuajiri watu wengi.