Home Kitaifa SERIKALI YAWATAKA WANANCHI BUTIAMA KUJIFUNZA ELIMU YA FEDHA

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI BUTIAMA KUJIFUNZA ELIMU YA FEDHA

Serikali imewataka Wananchi wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo ya elimu ya fedha ili kujiongezea maarifa yatakayowasaidia kusimamia vizuri rasilimali zao.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake, ambayo ipo mkoani Mara kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali.

Kushiriki katika mafunzo haya kutawawezesha wananchi kuepuka changamoto za kifedha kama vile madeni yasiyolipika, matumizi mabaya ya fedha, na kutokuwa na akiba ya kutosha kwa dharura,”, alisema Mhe. Kaegele.

Aliongeza kuwa wananchi wakijitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo ya elimu ya fedha kutawasaidia kupata maarifa yatakayowawezesha kufanya maamuzi bora ya kifedha na kujenga maisha yenye utulivu na mafanikio.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke Makanyanga, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na elimu muhimu ya fedha ili waweze kusimamia vizuri fedha zao.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, alisema kuwa wakati wanaendelea na zoezi la utoaji elimu katika makundi mbalimbali wamekutana na malalamiko kutoka kwa wananchi ambao wamekopa maeneo mbalimbali kubadilishiwa mikataba na watoa huduma wasiowaminifu.

Tumekutana na kesi mwananchi anasema kwenye mkataba aliosaini siku ya kwanza alikopa kiasi fulani, lakini anaporudi ofisini kutaka kuanza kufanya rejesho la kwanza anakuta mkataba mpya wenye kiwango kikubwa tofauti na alichokopa” alisema Bi. Elizabeth.

Alifananua kuwa ni haki ya mkopaji kuomba nakala ya mkataba wa mkopo ili utumike kama ushahidi iwapo kutatokea kubadilishiwa kiwango cha mkopo, lakini nakala hiyo itamsaidia mkopaji kujua taarifa muhimu ya kiwango cha riba, kiasi cha rejesho kila mwezi na kiasi cha mkopo alichokopa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!