Home Biashara TIGO NA INFINIX WAZINDUA INFINIX NOTE 12 VIP

TIGO NA INFINIX WAZINDUA INFINIX NOTE 12 VIP


Infinix washirikiana na Tigo kutambulisha simu mpya Note 12 VIP simu yenye uwezo mkubwa na sifa kedekede GB 256

Meneja wa mauzo wa vifaa vya intaneti wa Tigo Edwin Mgoa ( Kushoto )  akitambulisha simu mpya ya INFINIX NOTE 12 VIP  katika viwanja vya sabasaba ikiwa na Ofa ya Intaneti ya GB 96 BURE kutoka TIGO mwaka mzima , pembeni yake ni Erick Mkomaya Meneja Mahusiano Infinix Tanzania.

……………………………………………………*************************………………………………….

Leo tarehe 6 Julai 2022 , Kampuni namba moja ya huduma za Kidigitali hapa nchini Tigo,  kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu za mkononi Infinix wametambulisha simu mpya ya 4G aina ya Infinix NOTE 12 VIP.

Akizungumza wakati wa kutambulisha simu hiyo Meneja wa vifaa vya intaneti  kutoka kampuni ya Tigo Bwana Edwin Mgoa amesema simu hiyo itapatikana kwenye maduka ya Tigo na Infinix Nchi Nzima huku ikiwa na Ofa ya Intaneti ya GB 96  kwa mwaka, na kusisitiza juu ya dhamira ya Kampuni ya Tigo kuleta simu hizi nzuri na za kisasa ni kuhakikisha wateja wake wanakwenda kwenye mawasiliano ya Kidigital na kutimiza dhamira ya serikali ya kuhakikisha kwamba kufikia mnamo 2025 asilimia 80 ya vifaa vya mawasiliano vinakidhi TEHAMA kwa mfumo wa Kiserikali.

Naye Afisa Mahusiano Infinix Bwn. Eric Mkomaye amesema kuwa 

” Infinix NOTE 12 IP ina Processer  yenye speed Kali ya  G 96 itakayokuwezesha kucheza game, kuangalia movies mbalimbali kwenye internet kwa Kasi ya ajabu huku ukitumia Tigo

Note 12 pia Ina uwezo mkubwa wa camera kwa wapenzi wa picha na video ambayo camera yake Ina megapixels 108 na cinematic itakayokuwezesha kuchukua video katika mfumo wa films Pia Ina muonekano mzuri wa camera 3 kwa nyuma 

Sifa kubwa na ya kipekee Ina technologia ya milliamps wat 120 fast charge kwa dakika 17 tu inakua full charge na inakuja na charger yake maalumu ” Alimalizia.

Kujipatia Simu hii mpya ya Infinix NOTE 12 VIP tembelea maduka ya Tigo na Infinix nchi nzima

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!