Home Kitaifa MAJI YA KIMATAIFA YATUMIKE KULETA MAENDELEO-MHE. KADUARA

MAJI YA KIMATAIFA YATUMIKE KULETA MAENDELEO-MHE. KADUARA

Waziri wa Maji, Nishati na Madini Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Shahibu Hassan Kaduara amewataka watumiaji wa maji ya kimataifa kuwa waangalifu na wayatumie kwa matumizi sahihi na kwa usawa bila kuathiri matumizi kwa watumiaji wengine.
Mhe. Kaduara amesema hayo akifungua Kongamano la wadau wa maji ya kimataifa jijini Dar es Salaam.

Amesema maji ya kimataifa ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu hivyo yanapaswa kutumika kwa namna ambayo itasaidia pande zote ambazo zinachangia maji hayo ili kuleta maendeleoa na siyo kuleta ghasia.

Aidha amesisitiza majadiliano ya wadau yalenge kuhakikisha wanafikia makubaliano ambayo yatajenga umoja na mshikamano kwa wanachama.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema Wizara ya Maji iko tayari kushirikiana na mataifa yote katika suala la maji. Amesema kongamano hilo ni hatua ya awali ya majadiliano kuelekea kuikubali mikataba ya pamoja na nchi wanazochangia maji.

Amesema Tanzania ina jumla ya vyanzo vya maji ya kimataifa 14. Vyanzo hivyo ni pamoja na; ziwa Victoria ambalo liko Tanzania, Kenya na Uganda, Ziwa Nyasa, ZiwaTanganyika na Mito ukiwemo mto Nile.

Maji ya kimataifa ni maji shirikishi ambayo yanayovuka mipaka ya nchi moja kwenda nyingine, mfano maji katika ziwa Viktoria, Ziwa Nyasa na Mto Nile.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!