Home Kitaifa RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI

RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI

Na Mercy Maimu

Rais wa Tanzania, SAMIA SULUHU HASSAN ametunukiwa udaktari wa heshima (PhD) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Samia ametunukiwa udaktari huo leo Jumatano Novemba 30, 2022 na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Jakaya Kikwete katika mahafali ya 52 ya chuo hicho yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam

Kwa mamlaka niliyokabidhiwa, ninakutunuku digree ya heshima ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hongera sana” amesema Kikwete akimtunuku Rais Samia udaktari huo wa heshima.

Baada ya kutunukiwa udaktari huo, Rais Samia ameshukuru huku akibainisha alijaribu kuitafuta shahada hiyo lakini muda haukumpa nafasi.

Suala la kupewa tuzo hii nimelipokea kwa unyenyekevu mkubwa. Lakini nilijiuliza maswali kadhaa sababu huko nyuma nilijaribu kuitafuta shahada hii lakini muda haukunipa nafasi,” amesema Rais Samia

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!