Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEM David Silinde amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma Vijijini mkoa wa Mara Msongela Palela kuhakikisha mpaka ifikapo mwisho wa mwezi december mwaka huu awe amemaliza ujenzi wa maabara katika shule mpya ya sekondari katika kata ya Ifulifu ambayo walipewa milioni 470 ya ujenzi lakini mpaka kufika leo hii fedha hizo zimekwisha huku maabara hizo zikiwa bado hajimalizwa ujenzi wake.
Maagizo hayo ameyatoa akiwa katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa mapya mkoani humo na kukuta ujenzi wa madarasa katika wilaya ya Musoma ukiendelea vizuri na kutaka wakamilishe kwa wakati ili kuruhusu wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza waweze kuingia mapema mwakani katika mwaka mpya wa masomo january.
“Nakupa kipindi hiki cha wiki nne uwe umemaliza ujenzi wa maabara hizi maana wengine wote waliopokea fedha hizi za shule mpya za kata washamaliza kwa fedha hizo na elimu ya sasa inaitaji zaidi wanafunzi kujifunza kwa vitendo masino ya sayansi hivyo kama ulivyoniahidi hakikisha umekamilisha na mimi nitarudi tena kukagua mwezi ujao kama umekamilisha ujenzi huu” Silinde
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Silinde amewataka wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini kutuma taarifa kwa Waziri wa TAMISEM juu ya hali ya miradi yote ya shule mpya za kata ilipofikia mpaka sasa na ahadi yao ya kumaliza kabla ya mwezi january baada ya mda waliopewa wa ziada kumalizika huku baadhi ya halmashauri zikiwa hazijafanikiwa kumaliza ujenzi huo.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Musoma wa vijijini Msongela Palela amesema watatumia mapato ya ndani ya halmashauri zaidi ya milion 124 kumalizia ujenzi huo wa maabara kwa wakati.
Huku Katibu Tawala Mkoa wa Mara Msalika Robert Makungu amemuhakikishia Naibu Waziri Silinde maelekezo yote wameyapokea na kua mpaka ifikapo tarehe 15 mwezi ujao ujenzi wa madarasa yote mapya mkoa huo yatakua yamekamilika tayari kwa matumizi.