Na Magreth Mbinga
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa sugu anaefahamika kwa jina la Johnson Omary Mchome anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 39 ambae ni dereva wa bodaboda.
Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Murilo katika Mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa mwaka huu amekuwa akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya kiharifu katika maeneo mbalimbali pamoja na wenzake.
“Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu maeneo ya Kwembe katikati ya Kwembe na Kisarawe katika Wilaya ya Ubungo na kukamatwa kwake kulitokana na Wananchi wema kutoa taarifa ambazo zilifatiliwa kwa haraka na Makachero wa Jeshi la Polisi na mtuhumiwa huyu ambae wakati mwengine mitaani anatumia jina tofauti na lililopo katika kitambulisho cha mpiga kura pamoja na hati ya kusafiria ambapo mtaani anajulikana kwa jina la Athumani Rashidi Amir” amesema ACP Murilo.
Pia ACP Murilo amesema baada ya mtuhumiwa kubaini kuwa anafatiliwa na Jeshi la Polisi na amezingirwa alitoa Bastola kwenye begi na kuanza kuwashambulia Askari ambao nao walijihami kwa kumshambulia na kumpiga risasi moja katika mguu .
“Katika hali hiyo Askari walifanikiwa kuipata Bastola moja aina ya feth 13 ambayo ilikuwa na namba T 062010J004070 ambayo ilitengenezwa Uturuki ilikuwa na namba za usajiri za Tanzania TZ 95973 ambayo ilikuwa na risasi moja” amesema ACP Morilo.
Aidha ACP Murilo amesema ufatiliaji wa haraka wa Jeshi la Polisi ulibaini kuwa Bastola hiyo iliporwa eneo la Chanika ambapo waliwahi kufanya tukio wakiwa na mapanga wakafanikiwa kupora pesa katika moja ya nyumba pamoja na Bastola hiyo baada ya kumjeruhi kwa panga mmiliki.
“Mtuhumiwa huyu alihojiwa kwa kina zaidi na alieleza yeye pamoja na wenzake wamekuwa wakifanya matukio hayo mwaka huu kwenye maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam,kutokana na jeraha alilolupata mtuhumiwa amekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili keaajili ya matibabu na aweze kufanyiwa mahojiano baada ya kupona” amesema ACP Murilo.