Home Kitaifa RIDHIWANI KIKWETE AHIMIZA WELEDI KWA WATENDAJI WA ARDHI

RIDHIWANI KIKWETE AHIMIZA WELEDI KWA WATENDAJI WA ARDHI

Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwan Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze amefunga, Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka 2022 wa Taasisi ya Wapima Ardhi na Ramani (IST).

Katika kuhitimisha kongamano hilo mhe Naibu Waziri Ridhiwan amewahimiza watendaji husika kufanya kazi kwa kuzingatia taalum na weledi uliotuka ili kuendana na Sera ya Serikali ya awamu ya Sita ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wananufaika na ardhi.

Amewaasa wataaluma hao kuwa na utendaji bora kila mara kwani Nchi inawahitaji na kwamba serikali ipo tayari kushirikiana na wataalam hao katika kuleta maendeleo ya nchi.

Kongamano hilo lililenga uboreshaji utendaji mzuri sambamba na kuwakumbusha watalaam wa upimaji ardhi usio kuwa na upendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!