Home Kitaifa VETA YATAMBUA UJUZI KWA WANAGENZI 214 WALIOPO KATIKA VYUO VYA KUREKEBISHA TABIA.

VETA YATAMBUA UJUZI KWA WANAGENZI 214 WALIOPO KATIKA VYUO VYA KUREKEBISHA TABIA.

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Tanzania (VETA) CPA Anthony Kasore amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025 jumla ya Wanagenzi 5,175 walitambuliwa na kurasimishiwa ujuzi wao ikiwemo wanagenzi 214 waliopo kwenye vyuo vya kurekebisha tabia yaani wafungwa katika Magereza ya Ukonga,Arusha na Morogoro, na wengine 1,164 walikuwa ni wale wanaoshiriki miradi ya kimkakati ya ujenzi wa Reli ya Mwendokasi na Bwawa la umeme la Julius Nyerere ambao ilikuwa ni kupitia mpango wa Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi nje ya Mfumo rasmi.

CPA Kasore ameyasema hayo Machi 3,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Dkt Samia.

Na kusema kuwa Bodi wamesimamia vizuri na kuweka kwenye mpango Programu ya Mama Samia ya urasimishaji wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi ambapo mafundi mahiri na waliobobea hujengewa uwezo na kupatiwa vyeti vinavyoonesha maeneo ya mahiri zao, huku Veta ikijipanga kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo kwa vijana 80,000 nchini ifikapo June 2026.

Kupitia Mpango wa Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi (Recognition for Prior Learning) uliopatikana nje ya mfumo rasmi, katika kipindi cha Mwaka 2021 hadi 2025, jumla ya wanagenzi 5,175 walitambuliwa na kurasimishiwa ujuzi wao. Kati yao wanagenzi 1,164, walikuwa wanaoshiriki miradi ya kimkakati ya Ujenzi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) na Bwawa la la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) na 214 waliopo kwenye vyuo vya kurekebisha tabia (wafungwa katika Magereza) vya Ukonga, Arusha na Morogoro. Aidha, ili kuendana na Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2021/2022 – 2025/2026 unaoelekeza urasimishaji wa ujuzi kwa mafundi 100,000 ifikapo Juni 2026, Pamoja na ilani ya chama tawala VETA imepanga
kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo kwa vijana 80,000 nchini ifikapo June 2026
“.

Bodi wamesimamia na kuweka kwenye mpango Programu ya mama Samia ya urasimishaji wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi, ambapo mafundi mahiri/waliobobea hujengewa uwezo na kupatiwa vyeti vinavyoonesha maeneo ya mahiri zao”.

Katika suala la uendelezaji wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasilano,CPA Kasore amesema Veta inatumia vifaa vya TEHAMA kutoa mafunzo kwa mfumo wa elimu masafa pamoja na kutumia Teknolojia za kisasa katika ufundishaji na ujifunzaji.

VETA inaendelea kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasilano (TEHAMA) katika ufundishaji na ujifunzaji wa mafunzo ya Ufundi stadi. Kwa sasa VETA inatumia Mfumo wa VSOMO ambapo wanafunzi wanajifunza kwa nadharia kupitia mfumo huo kwenye simu janja na baadae kuhudhuria mafunzo kwa vitendo Vyuoni na Viwandani. Vilevile, VETA inatumia vifaa vya TEHAMA kutoa Mafunzo kwa mfumo wa elimu masafa (Open and Distance eLearning-ODeL). Hali kadhalika VETA imeanza kutumia Teknolojia za kisasa katika ufundishaji na ujifunzaji. Tekinolojia hizo ni Pamoja na Virtual Reality Technology, Simulators, Mechatronics, Robotics, Artificial Intelligence (Akili Unde) na Internet of Things (IOT)“.

Katika matumizi ya Simulators Serikali imetumia Shilingi milioni 273 kununua vifaa hivyo kwa ajili ya mafunzo ya uchomeleaji na uungaji vyuma“.

Aidha amesema kuwa ili kupanua wigo wa kudahili wanafunzi Serikali imeiwezesha VETA kuongeza idadi ya vyuo vya ufundi stadi nchini kutoka vyuo arobaini na moja mwaka 2020 hadi kufikia vyuo 80 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100 ya vyuo vya ufundi stadi nchini linalolenga kuiwezesha VETA kushiriki kikamilifu katika kufikia malengo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2025/2026 kwa kuongeza nguvukazi mahiri kwa maendeleo ya Uchumi wa Taifa.

Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita (2021 hadi 2024), jumla ya vijana 295,175 wamedahiliwa katika vyuo vya VETA katika kozi za muda mrefu na muda mfupi. Ili kupanua wigo wa kudahili wanafunzi Serikali imeiwezesha VETA kuongeza idadi ya vyuo vya ufundi stadi nchini kutoka vyuo arobaini na moja (41) mwaka 2020 hadi kufikia vyuo themanini (80) mwaka 2025. Ongezeko hili la takribani asilimia 100 ya vyuo vya ufundi stadi nchini linalenga kuiwezesha VETA kushiriki kikamilifu katika kufikia malengo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26 kwa kuongeza nguvukazi mahiri kwa maendeleo ya Uchumi wa Taifa. Aidha hadi kufikia Juni 2026 vyuo vipatavyo 65 vinategemewa kukamilika na kuanza kutoa mafunzo. Hivyo kupelekea VETA kuwa na jumla ya vyuo 145 nchini. Ongezeko hili la vyuo linategemewa kuongeza udahili hadi kufikia wanafunzi 200,000 kwa mwaka.Mitaala”.

Na kuongeza Veta imehuisha Mitaala 42 na kuanzisha mitaala mipya 20 katika Sekta za TEHAMA, Michezo,Umeme,Magari,Mitambo,Kilimo,Ukarimu, Usafirishaji, Biashara, Mavazi, Madini,na Urembo yote ikiwa na lengo la kuiwezesha VETA kukidhi mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya teknolojia.

VETA imehuisha mitaala 42 na kuanzisha mitaala mipya 20 katika sekta za TEHAMA, Michezo, umeme, magari, mitambo, kilimo, ukarimu, usafirishaji, biashara, mavazi, madini, na urembo. Uhuishwaji na uanzishwaji wa mitaala hiyo 62 ulilenga kuiwezesha VETA kukidhi mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya teknolojia ili kuandaa wahitimu wenye ujuzi unaohitajika ndani na nje ya nchi sambamba na utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo la Mwaka 2023) inayosisitiza kuhusu Elimu Ujuzi.

Itakumbukwa kuwa tarehe 22 mwezi Aprili, 2021 Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipohutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisisitiza kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na kufanya maboresho kwenye mitaala iliyopo ili ielekezwe kwenye kutoa elimu ujuzi kulingana na mazingira ya nchi na soko la ajira.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!