Home Kitaifa ASKOFU “DAO” KUTUMIA REDIO MPYA MUSOMA TETEMO FM KUINUA VIPAJI VYA SANAA...

ASKOFU “DAO” KUTUMIA REDIO MPYA MUSOMA TETEMO FM KUINUA VIPAJI VYA SANAA YA VIJANA

Na Shomari Binda-Musoma

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church Tanzania( NLGCCT) Daniel Ouma maarufu kama (Askofu Dao) amesema ataitumia redio mpya itakayowashwa Musoma mwishoni mwa mwezi huu wa 3 kuinua vipaji vya sanaa ya vijana.

Kauli hiyo ameitoa jana februari 28 wakati akifungua fainali za mashindano ya kusaka vipaji vya sanaa ya vijana ya Musoma Samia Talent Search msimu wa kwanza 2025.

Mashindano hayo yaliyodumu kwa wiki 5 yalikuwa yakihusisha kuibua vipaji vya uimbaji,uchekeshaji pamoja na uchezaji.

Akizungumza na washiriki walioingia hatua hiyo ya fainali na watazamaji kwenye ukumbi wa Serengeti Resort amesema kupitia sanaa ya vijana hao wanaweza kuikumbusha jamii kumkumbuka Mungu kupitia kile wanachokionyesha jukwaani

Amesema yeye kwa kuwa ni mkurugenzi wa kituo cha redio kinachokwenda kuanzishwa kutakuwa na kipindi cha kuibua na kuendeleza vipaji.

Askofu huyo amesema wapo wasanii wenye vipaji vya uimbaji wa nyimbo za dini ambao utumia vipaji vyao kuifikia jamii kuweza kumjua Mungu na kumuabudu

Aidha amesisitiza kuwa na nidhamu kwa wasanii hao kwa kuwa sanaa sio njia ya kufanya uhuni kwani ni ajira za kipaji na wapo walionufaika kupitia sanaa wanazozifanya.

” Nimekuja hapa kuwatia moyo nikiamini sanaa mnayoifanya mtaikumbusha jamii kumjua Mungu na kumuabudu nanyi mkapata kipato.

” Nimshukuru na kumpongeza mkurugenzi wa Yeguwasu Tv Online Daniel Mabuba kwa kuanzisha jukwaa hili nasi tutashirikiana nae kuona hiki anachokifanya kuwasaidia vijana kinaendelezwa”,amesema.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Yegowasu Tv Online inayorusha maudhui mtandaoni Daniel Mabuba amesema ameona Musoma hakuna jukwaa la kuibua vipaji na kuamua kuanzisha jambo hilo.

Amesema mwanzo umekuwa mzuri kwa vijana wengi kujitokeza kushiriki na wadau mbalimbali kusaidia kufanikisha kufanyika kwake.

Katika msimu huu wa kwanza msanii aliyeibuka mshindi kwenye eneo la uchekeshaji ni Mwita Mwita,uimbaji ni Official Joy na kundi bora la uchezaji ni Shadow Geng dancers ambao wote walikabidhiwa zawadi za kufanya vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!