Home Kitaifa RAIS SAMIA: MIRADI MIKUBWA KICHOCHEO CHA AJIRA KWA VIJANA

RAIS SAMIA: MIRADI MIKUBWA KICHOCHEO CHA AJIRA KWA VIJANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiendelea na ziara yake mkoani Tanga, amesema kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchini itachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ajira kwa vijana.

Akizungumza na wananchi wa Tanga leo(Februari 28, 2025), Rais Samia amesema:

Kupitia miradi mbalimbali ya BBT ile ya vijana pamoja na mradi mkubwa wa Mkomanzi, tutatengeneza ajira nyingi kwa vijana.

Ameongeza kuwa serikali inaendelea kurahisisha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wakubwa, hatua inayolenga kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Aidha, Rais Samia amesema kuwa amezindua kiwanda cha chokaa na saruji cha Mwawene Limestone, ambacho kimepanuliwa, na upanuzi huo umeongeza ajira mpya 824, ambapo 424 ni ajira za moja kwa moja na 400 ni ajira zisizo za moja kwa moja.

Viwanda vya aina hii vitaendelea kuanzishwa ili kuhakikisha vijana wanapata ajira na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi,” amesema Rais Samia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!