Home Kitaifa RAIS SAMIA AZINDUA MWONGOZO WA MATUMIZI YA MATOKEO YA SENSA YA WATU...

RAIS SAMIA AZINDUA MWONGOZO WA MATUMIZI YA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua muongozo maalumu kwa matumizi ya matokeo Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa lengo la kuongeza uelewa,uwazi na kupanua wigo wa matumizi ya matokeo ya sensa kwa mwaka 2022 katika kupanga mipango ya maendeleo ya kijamii,kiuchumi na kimazingira ambapo utatumika kwanzia Nov 2022 hadi Oct 2032.

Rais Samia ameyasema hayo leo 31 oktoba,2022 wakati akizindua matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi Jijini Dodoma.

Muogozo huu ni wakwanza kuandaliwa tangu tulipopata uhuru na wakwanza katika bara la Afrika kwenye mzungukowa umoja wa mataifa wa kufanya sensa ya makazi katika miaka ya 2020 inawezekana wapo watakaofanya kama tulivyofanya sisi lakini sisi ni wakwanza kufanya kufanya hivi” Amesema Rais Samia.

Pia Amesema kuwa idadi iliyopatikana kwa mwaka 2022, ni 61,741,120 Tanzania kwa ujumla ambapo Bara inajumla ya watu 59,851,347 na zanzibar 1,889,773 jumla yawanawake ni 31,687,990 ( 51%), na wanaume 30,053,130 ( 49%.). Ambapo limepatikana Ongezeko la 3.2% Tanzania bara na 3.7%zanzibar Tangu 2012. huku mkoa wa Dar es salaam na Mwanza zikiongoza kwa watu wengi nchini.

Rais Samia amesema kuwa taarifa za sensa ya watu na makazi inaumuhimu kwa kufuatilia na kutathmini sera na mipango miji na kuwezesha kufikia wananchi huku akiwataka viongozi na wananchi kutumia taarifa hizo kwa dhumuni lililokusudiwa ambalo ni kuboresha maisha ya kila mtanzania.

Aidha Rais ya Zanzibar Dkt. Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa serikali itapanga na kutekeleza mipango ya Nchi kwa kuzingatia ushahidi wa kitakwimu ili maamuzi hayo yawe yanaakisi hali halisi kwa maana idadi ya watu na mahitaji yao.

Rais Samia ametoa wito kwa viongozi ili matokeo ya sensa yaanze kutumika katika kupanga miradi ya wananchi,bajeti,sekta,binafsi na wawekezaji wote wa mioango jumuishi ya maendeleo endelevu kwa Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!