Home Kitaifa WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MAKTABA MPYA YA UONGOZI ILIFASIRI KITABU CHA HAYATI BENJAMINI...

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MAKTABA MPYA YA UONGOZI ILIFASIRI KITABU CHA HAYATI BENJAMINI KWA LUGHA YA KISWAHILI

Na Magrethy Katengu

Waziri Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amewataka watanzania hususan viongozi mbalimbali, kujenga utaratibu kutumia maktaba hiyo mpya kupata maarifa kwa kusoma na kuandika vitabu kwa lugha ya Kiswahili ili kuchagiza utekelezaji wa mipango ya taifa, na kubadili fikra za watanzania.

Waziri Mhagama ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Maktaba ya Uongozi na Utambulisho wa toleo la Kiswahili la kitabu cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa cha ‘Maisha yangu kusudio langu’ kwa lengo la kusaidia watanzania wote wasioelewa lugha ya kingereza kupata fursa ya kukisoma kwa kiswahili.

Hata hivyo amesema kuwa machapisho na vitabu vingi nchini vina mitazamo na tamaduni za nchi za kimagharibi na lugha za kigeni, hivyo ili kuondoa dhana ya kuwa watanzania kukosa utaratibu wa kusoma vitabu kwa kigezo cha kutoelewa lugha, waandishi wa vitabu wanatakiwa kujikita zaidi kuandika vitabu vyao katika lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia maadili na tamduni za Mtanzania.

Wote tunafahamu kuwa Maktaba ni chombo muhimu cha kutolea maarifa zilizohakikiwa kiuchumi,Kijamii na kisiasa na zikiifikia Jamii zina mtazamo wa kubadilisha mawazo” amesema Waziri

Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Mke wa Hayati Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa amesema kuwa hatua ya uzinduzi wa maktaba ya uongozi na utambulisho wa toleo la Kiswahili la kitabu cha Hayati Rais Benjamini Mkapa kwani kabla ya kufariki ilikuwa ni lengo lake kubwa wakati akizindua kitabu hicho kwa lugha ya kingereza kifasiriwe kwa kiswahili.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi ya Uongozi, Balozi Ombeni Sefue, amesema kuwa viongozi na watanzania kwa ujumla wanapaswa kumtendea haki Hayati Rais Mkapa kwa kusoma kitabu hicho alichokiandika kwa ajili ya ila mtanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!