Home Kitaifa WAMKELE MENE AITAKA AFRIKA KUONDOKA VIKWAZO VYA KIBIASHARA; VIJANA, WAJASIRIAMALI WAPEWE KIPAUMBELE

WAMKELE MENE AITAKA AFRIKA KUONDOKA VIKWAZO VYA KIBIASHARA; VIJANA, WAJASIRIAMALI WAPEWE KIPAUMBELE

Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) Mhe. Wamkele Mene ametoa rai kwa Afrika kuungana na kuondoa vikwazo vya kibiashara, na kutoa kipaumbele kwa vijana, wajasiliamali wadogo na wafanyabiashara ili kukuza uchumi wa nchi za kiafrika.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo Julai 03, 2022 alipokuwa akifungua Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalianza tarehe 28 Juni hadi 13 Julai 2022 katika uwanja wa Mwl J. K. Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Akimkaribisha Katibu Mkuu Huyo , Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema kutokana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuimarisha mazingira rafiki ya Uwekezaji na Biashara katika fursa mbalimbali. Kampuni 3,380 zimevutiwa kushiriki katika maonesho hayo ambapo kampuni 3,200 ni za Kitanzania na 180 ni za nje kutoka katika nchi 21

Aidha, Maonesho hayo yamejumuisha tunaratibu Programu ya Total Industrial Solution ambapo mitambo mbalimbali inayoweza kukamilisha viwanda vidogo na vya kati ambapo Mjasiriamali anaweza kumiliki mitambo hiyo inayoanzia thamani ya milioni 6 hadi milioni 600. Amesema.

Waziri Kijaji, amesema Maonesho hayo yanaongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Tanzania: Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji” ikilenga kutambua umuhimu wa mchango wa Sekta ya Uwekezaji na Biashara katika kukuza na kuimarisha Diplomasia ya Uchumi baina ya Tanzania na nchi nyingine.

Naye Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameimarisha mahusiano na mataifa ya nje kwa kuondoa vikwazo vya kibiashara hivyo ametoa wito kwa ya nje ya Afrika.ametoa rai kwa Watanzania kuzalisha kwa amesema wingi na kuilisha bara la Afrika na mataifa.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godus Kahyarara amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameimarisha mahusiano yetu na mataifa ya nje kwa kuondoa vikwazo vya kibiashara hivyo natoa wito kwa watanzania kuzalisha kwa wingi na kuilisha bara la Africa na mataifa ya nje ya Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!